Habari za Punde

Michuano ya Mapinduzi Cup Timu yaYanga Yaibuka Kidedea Yaifunga Timu KVZ Bao. 1- 0 Usiku Huu Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Mshambuliaji wa Timu ya KVZ  Raphael Obi, akijaribi kumpita beki wa Timu ya Yanga Clefa Sospeter, wakati wa mchezo wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika usiku katika Uwanja wa Amaan Zanzibar, Timu ya Yanga imeshinda mchezo huo bao 1-0, 
Lililofungwa na mshambuliaja wake Shaban Mohammed katika dakika ya 75 ya mchezo huo kipindi cha Pili. baada ya kuunganisha krosi iliopigwa na beki Haji  Mwinyi.
Beki wa Timu ya Yanga Clefa Sospeter akiwani mpira na mshambuliaji wa Timu yua KVZ Ayuob Lipati, wakati wa mchezo wao kuwania Kombe la Mapinduzi mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Timu ya Yanga imeshinda mchezo huo kwa bao 1-0.
Mshambuliaji wa Timu ya KVZ na wa Yanga wakiwania mpira wakati wa mchezo wao Michuano ya Kombe la Mapinduzi Uliofanyika Uwanja wa Amaan Zanzibar. Timu ya Yanga imeshinda mchezo huo kwa bao.1-0. 
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga Shaban Mohammed akishangilia bao lake katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi uliofanyika katika Uwanja wa Amaan Zanzibar usiku huu, na Kuiwezesha Timu yake kutoka kivua mbele na kuongoza kundi lao. 
Wachezaji wa Timu ya Yanga wakimpongeza na kushangilia bao lao la kwanza lililofungwa katika dakika ya 75 na mshambuliaji wake Shaban Mohammed.


Mwandishi wa Habari za michezo wa Kituo cha TV cha Azam Bin Zubery, akimuhoji mshambuliaji wa Timu ya Yanga Shaban Mohammed, aliyeiandikia bao la ushindi Timu yake katika dakika ya 75 ya mchezo huo kipindi cha pili, wakati wa michuano ya Kombe la Mapinduzi, uliofanyika usiku huu katika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Meneja wa Timu ya Yanga Haroub Kanavaro akizungumza na waandishi wa habari za michezo wanaoripoti habari za michezo Kombe la Mapinduzi, Timu yake imeshinda bao 1-0 na kuongoza katika kundi lao. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.