Habari za Punde

Wadau wa Mradi wa Uwajibikaji wa PAZA Zanzibar Wamepata Mafanikio Makubwa Kupitia Mradi Katika Kipindi Kifupi.



Na.Thabit Madai Zanzibar.   

Wakizungumza katika mkutano huo walisema kuwa mradi huo umewawezesha kujua mambo mengi ambayo yalikuwa yamejificha sambamba na kuwafikia jamii kuwaelezea jinsi ya kutoa taarifa wanapokuwa na changamoto.

Mwanajuma Kassim kutoka Jumuiya ya Wanawake ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa Kijinsia ya Mkoa wa Kaskazini alisema kuwa kupitia mradi huo wameweza kufika vijijini na kuweelezea watu juu ya kuzijua haki zao za msingi.

Alisema kuwa wengi wa wananchi walikuwa wakidhani kuwa haki zao za msingi ni zile zilizozoeleka ikiwemo kula, kuvaa na kuishi katika mazingira mazuri jambo ambalo kupitia mradi huo wameweza kupata zaidi.

“Kwa kipindi cha mwaka mmoja na kazi tulizozifanya tumefanikiwa sana tunaipongeza sana TAMWA kupitia mradi huu kwa hatua walizochukuwa mpaka tukafikia hapa”, alisema Mwanajuma.

wa Hata hivyo alisema pamoja na kuwa mradi huo haujamalizika kwa mradi huo kuna haja ya kuendelea kufatilia pale ambapo walipofikia na kuziomba Halmashauri kuwaingiza katika miradi yao wanayoyapanga.

“Wapo wanawake mpaka leo hawajui kwamba katika Halmashauri zao kuna haki zao kwa kuwepo miradi ambayo na wao wanahitaji kushirikishwa kwa hiyo ni vyema halmashauri zinapoandaa mipango yao na sisi watushirikishe”, alisema.

Hata hivyo baadhi ya watendaji katika Halmashauri waliokuwepo kwenye mkutano huo walisema kuwa kuibuka kwa changamoto katika vijiji hakumainishi kwamba hakuna uwajibikaji.

Ali Abdu Ali Afisa Maji wilaya ya Kati Unguja alisema kuwa  kuna changamoto nyingi zinajitokeza lakini nyengine zinakuwa nje ya uwezo wao jambo ambalo alisema kuwa ni vyema wakaungana kwa pamoja na kuweza kuzifanyia kazi.

“Mie landa niseme tu kwamba si kila linaloibuliwa kuwa changamoto kwamba hakuna uwajibikaji kwa viongozi la hasha bali kuna changamoto nyengine zinakuwa bado hazijafikiwa na bajeti yake”, alisisitiza.

Akifunga mkutano huo Meneja Miradi wa TAMWA Asha Abdi Makame alisema kuwa ni wajibu kila mwananchi kwenda kufatilia matatizo yaliyomo katika vijiji vyao ili kuweza kufanyiwa kazi.

Alisema kuwa mradi huo wa Uwajibikaji unaisha lakini changamoto ambazo zimeibuliwa bado zipo na zitaendelea kuwepo hivyo ni jukumu la kila mmoja wao kuona wanazifatilia na kuzifanyia kazi kwa maendeleo ya sasa na baadae.

Mradi wa Uwajibikaji unadhaminiwa na EU ambao unafanyika kwa mashirikiano ya karibu kati ya TAMWA , Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo (WAHAMAZA) na Jumuiya ya Kuhifadhi Mazingira  Pemba (NGERENEKO

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.