Habari za Punde

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Azindua Jengo la Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar.

Muonekana wa Jengo la Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI) liliopo Binguni ambalo lilifunguliwa rasmi na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Hassan ikiwa miongoni mwa maadhimisho ya mika 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Hassan akikagua jengo la Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar liliopo kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati baada ya kuluizindua rasmi ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Asha Abdalla Juma akitoa maelezo ya ujenzi wa Jengo la Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI) na kumkaribisha Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Hassan kuzungumza na wananchi baada ya kulizindua jengo hilo katika kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Hassan akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa Jengo la Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI), katika kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Binguni walioshiriki uzinduzi wa Jengo la Taasisi ya Utafiti wa Afya (ZAHRI) wakimsikiliza Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Hassan (hayupo pichani)  
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Hassan (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar (ZAHRI) baada ya kulizindua jengo hilo katika kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati. 
Na.Khadija Khamis – Maelezo  Zanzibar.
Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Ibrahim Raza amesema ushirikiano wa wananchi na viongozi wa jimbo ndio hatua bora inayoleta ufanisi wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya kuhakikisha ahadi zilizotolewa zinatekelezwa kwa vitendo.
Aliyasema hayo huko katika kiwanja cha mpira cha Kwala, Mombasa, wakati akizungumaza na waandishi wa habari walipofika kuangalia Taa zilizowekwa katika kiwanja hicho na kukiwezesha kutumika wakati wa usiku
Taa hizo zimewekwa kwa ajili ya kuwapa fursa vijana kucheza wakati wote na kukuza vipaji walivyanavyo na hatimae kupata nafasi ya usajili kwa vilabu vikubwa.
 Mwakilishi wa Jimbo la Kiembe samaki Mahamoud Thabit Kombo alisema baada ya kiwanja hicho kuwekwa taa, wanampango wa kukiimarisha zaidi kwa kukiweka nyasi badia.
Alisema lengo ni kuimarisha michezo katika jimbo la Kiembesamaki ikiwa ni moja ya njia ya kutengeneza ajira kwa vijana na kuwaepusha na vitendo viovu.
Aliwataka vijana wanaoishi karibu na kiwanja hicho kuwa walinzi wa raslimali iliyowekwa ili kidumu kwa muda mrefu na kiweza kutumiwa na vizazi vya sasa na vinavyokuja
Mwenyekiti wa C.C.M Jimbo la Kiembe Samaki Ramadhani Mrisho Rupia alisema kuimarisha michezo ni moja ya ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kuwasaidia vijana kujiajiri kutokana na vipaji walivyonavyo .
Taa za kiwanja cha mpira cha Kwala zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi Februari 22, mwaka huu kwa mechi maalum itakayofanyika wakati wa usiku.
Nae kijana Nasir Ali Hemed  Mkaazi wa kwa Mchina ambae ni mmoja ya vijana wanaotumia kiwanja cha Kwala , alisema amepata faraja  kuona viongozi wao wametekeleza ahadi zao kwa vitendo.
Aliwaomba viongozi wa Jimbo hilo kuwapatia mashine ya kukoshea gari (Presha Pampu) ili vijana waweze kujiajiri wenyewe
Jumla ya shiling milion 20 zimetumika kwa ajili ya kuweka miundombinu ya umeme katika kiwanja hicho

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.