Mwanasheria wa Chama cha cha
Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga (TAWLA) Mwanaidi Kombo akisisitiza
jambo wakati wa mafunzo hayo
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada
mbalimbali kwenye mafunzo hayo
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada
mbalimbali kwenye mafunzo hayo
Mmoja
wa washiriki wa Mafunzo hayo Michael Guni akiuliza swali
wakati wa mafunzo kwa
wasaidizi wa Kisheria wa wilaya za
Tanga ,Muheza na Pangani yaliyofanyika Jijini Tanga.
KUTOKUANDIKWA wosia kwa baadhi ya jamii mkoani Tanga
kumetajwa kuwa ndio chanzo kikubwa cha migogoro mingi ambayo imepelekea
mipasuko ambayo inachangia familia nyingi kutengana kutokana na
kugombania mali imeelezwa
Hayo yalisemwa na Mratibu wa Chama cha Wanasheria
Wanawake Mkoani Tanga (TAWLA) Wakili Latifa Ayoub wakati wa mafunzo kwa
wasaidizi wa Kisheria wa wilaya za Tanga ,Muheza na Pangani .
Mafunzo hayo yalilenga juu ya upatikanaji wa haki kwa
wanawake katika kumiliki kupata na kutumia ardhi na uelewa juu ya sheria
ya utoaji wa msaada wa kisheria kwa wasaidizi hao jana yaliyoratibiwa
na chama hicho.
Kwa mujibu wa mratibu huyo alisema uandikaji wa wosia ni
mzuri kutokana na kwamba umekuwa ukipunguza migogoro ndani ya familia
wakati aliyekuwa akimilika mali husika anapofariki dunia iwapo
utaandikwa kihalali.
“Kutokana na kuonekana kuwepo kwa changamoto hii ya
uandikaji wosia jamii sisi kama Tawla tulianza kuandika wosia tokea
mwaka 2007 lengo kubwa likiwa ni kupunguza migogoro mikubwa pindi mtu
anapokuwa akiondoka duniani”Alisema.
Aidha alisema tokea walipoanza kufanya hivyo mpaka sasa
wamekwisha kuandika wosia kwa watu 10 lakini bado wanaendelea na suala
hilo hivyo jamii inaweza kuchangamkia fursa hiyo iwapo itaaona kuna
umuhimu wa kuandika
“Lakini hapa cha muhimu kuandika ni kuwapatia elimu jamii
waweze kujua kuandika changamoto ni wanaotaka kufanya hivyo ni wazee
wakati mwengine hawafiki ofisini na hivyo kuhitaji kufuatwa”Alisema
Pia alisema bado mwamko ni mdogo sana kwa watu kuandikia
wosia jambo ambalo wakati mwengine linachangiwa na imani za dini kwa
baadhi ya watu huku wengine kutokuwa na uelewa.
Alieleza wanashindwa kuelewa mali mbalimbali wanazomilika
ikiwemo baiskeli ,shamba na nyumbazote hizo ni mali ambazo mtu anaweza
kuandika wosia ikiwa anafariki dunia ili wahusika wanaobakia kuepukana
na migogoro.
“Kutokana na kuwepo kwa mwamko huo mdogo sasa tutalazimika
kuendelea kutoa elimu kueleza namna ya waweze kuandika wosia kwa lengo
la kuepusha mipasuko na mifarakano kwenye jamii hususani mwenye mali
anapofariki dunia “Alisema Mratibu huyo Wakili Latifa.
Awali akizungumza wakati wa Mafunzo hayo mmoja wa washiriki
Michael Guni alisema mafunzo hayo yamewapa mwanga kuweza kutekeleza
wajibu wao wa kila siku katika utoaji wa haki hususani kwa wanawake
katika kupata na kumiliki Ardhi.
No comments:
Post a Comment