Habari za Punde

Kamati ya maendeleo BLW yaridhishwa na Serikali kuwapatia wananchi maeneo ya makaaza Dunduma

Na Mwashungi Tahir          Maelezo    

Kamati ya Maendeleo ya Baraza la Wawakilishi imeridhishwa na hatua iliyofikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kuwapatia maeneo ya makaazi  wananchi Dunduma eneo la Gongoni Shehia ya Kidanzi.
Hayo aliyasema huko Mangapwani Makamo Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi na Mawasiliano Baraza la Wawakilishi Suleiman Farahani wakati walipokuwa wakifanya ziara ya kutembelea katika maeneo hayo yaliyotengwa kwa ajili ya kuwekewa makaazi .
Alisema Serikali ya Mapinduzi  chini ya uongozi wake Dkt Shein  inaendelea kutimiza  ahadi zake kwa wananchi wake katika kuwaletea maendeleo na kuwawekea mazingira yaliyo safi  ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi .
“Hii ni azma ya serikali chini ya uongozi wa Dkt Shein kuhakikisha wanancho wote wanaishi katika mazingira mazuri na yaliyo bora,” alisema Mwenyekiti huyo.
Aidha  alisema wananchi wameridhika kwa hatua iliyochukuliwa na Serikali kwa kupatiwa sehemu ya makaazi ya uhakika na hakuna mwananchi aliyetoa  malalamiko kwa sababu tayari wameshatayarishiwa mazingira mazuri  ya maisha yao.
Alishukuru  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma Nishati na Maji ( ZURA ) kwa  kusimamia vya kutosha maendeleo ya ulipaji fidia kwa wananchi wa maeneo hayo upitia Wizara ya Ardhi , Nyumba, Maji na Nishati pamoja na Serikali kwa kutimiza lengo lililokusudiwa.
Nae Waziri Wa   Ardhi Nyumba Maji na Nishati Salama Aboud Talib  alisema anatoa shukurani kwa  mashirikiano aliyoyapata kwa mawaziri wenziwe wakiwemo Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na  Usafirishaji, Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Wizara Maalum ya SMZ pamoja na Wizara ya Fedha kukamilisha kazi hiyo.
Pia aliwataka wananchi wa eneo hilo kuwa na utulivu kwani tayari Serikali  ishafanya tathmini na ishatenga  fedha kwa ajili ya ujenzi huo ambapo unakadiriwa kumalizika kwake baada ya miezi sita.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Hu duma Nishati na Maji ZURA Hemed Salim amesema wananchi wa hapo watajengewa nyumba za kisasa na za uhakika na pia huduma zote za jamii zitakuwepo ikiwemo soko, skuli, msikiti na madrasamaduka, zahanati  , Uwanja mkubwa , barabara na tayari washakabidhiwa vikosi kwa ajili ya ujenzi KMKM na Mafunzo.
Alisema mpango wa Serikali ni kuwajengea wananchi nyumba safi kwa lengo ya kuwawekea sawa mazingira yaliyo bora na mazuri ili waishi kwa aqmaqni wao na familia zao .
Kamati hiyo pia ilitembelea sehemu inayotarajiwa kujengwa bandari ya kisasa huko Mangapwaniambayo itakuwa inashughulikia mafuta na gesi asilia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.