Habari za Punde

Uzinduzi wa Mradi Mpya Unaowashirikisha Wanafunzi wa Kike na Wanawake Wanaoishi na Maradhi Yasioambukiza.

Kaimu Meneja wa Kitengo cha maradhi yasiyoambukiza Wizara ya Afya Zanzibar Omar Abdallah Ali (kulia) Mwenyekiti wa Z-NCD Said gharib Bilal akitoa tarifa ya uchunguzi wa maradhi yasiyoambukiza katika Tamasha la vyakula vya asili lilifanyika Makunduchi mwaka jana.
Makamu mwenyekiti wa Jumuiya ya Maradhi Ysiyoambukiza Zanzibar Ali Zubeir Juma akitoa ufafanuzi wa maswali ya wandishi wa habari (hawapo pichani).
Mratibu wa Jumuiya ya maradhi yasiyoambukiza Zanzibar (Z-NCDA) Haji Khamis akitoa tarifa ya mradi mpya wa afya kwa wanafunzi wa skuli za Sekondari za Wilaya ya Mjini Unguja.
Baadhi ya wandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano wa Z-NCDA uliofanyika ofisi ya Jumuiya hiyo Mpendae.
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar.
Jumuiya ya maradhi yasiyoambukiza Zanzibar (ZNCDA) inaendesha Mradi mpya wa mwaka mmoja ulioanza mwezi Novemba mwaka jana na unawashirikisha Wanafunzi wa kike wa Skuli za Sekondari za Serikali za Wilaya ya Mjini na Wanawake wanaoishi na Maradhi yasiyoambukiza
Akiutangaza Mradi huo mbele ya waandishi wa habari katika Ofisi ya ZNCDA Mpendae, Mratibu wa Jumuiya hiyo Haji Khamis alisema lengo la Mradi huo ni kuwawezesha wanafunzi wa kike wa skuli za sekondari na wanawake wanaoishi na maradhi yasiyoambukiza.
Alizitaja skuli 17 zinazoshiriki katika mradi huo ni Bembella, Chumbuni, Faraja, Forodhani, Haile selassie, Hamamni, Hurumzi, Jangombe, Kidongochekundu, Kiponda, Kwamtipura, Lumumba, Mikunguni, Mpendae, Mwembeladu, Nyerere na Vikokotoni.
Alisema shughuli za Mradi huo ni pamoja na kutoa mafunzo ya uelimishaji rika kwa wanafunzi wa kike, kutayarisha vipeperushi vinavyohusu uhusiano wa afya ya uzazi na maradhi yasiyoambukiza na umuhimu wa kushiriki chanjo ya kinga ya Saratani ya mlango wa kizazi.
Mratibu wa ZNCDA Haji Khamis alisema mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Muungano wa Jumuiya za watu wa Denmark kupitia watu wanaoishi na maradhi yasiyoambukiza la nchi hiyo, unalenga kuwafikia wanafunzi wa kike 2,000 wenye umri wa miaka 14.
Wakati huo huo Kaimu Meneja wa Kitengo cha maradhi yasiyoambukiza Wizara ya Afya Zanzibar Omar Abdalla amesema ushirikiano wa pamoja unahitajika katika kukabiliana na maradhi yasiyoambukiza ili kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na maradhi hayo.
Alisema taarifa ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) ya mwaka jana asilimia 71 ya vifo vinavyotokea duniani vinatokana na Maradhi yasiyoambukiza na vingi vinatokea katika umri wa miaka 30 hadi 69 na mataifa ya Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Zanzibar zinaathirika zaidi.
Alivitaja vichocheo vikubwa vinavyosababisha maradhi yasiyoambukiza kwa Zanzibar kuwa ni mlo usiokamili, kutokufanya mazoezi utumiaji wa vyakula vyenye chumvi na mafuta kwa wingi.
Akitoa taarifa ya uchunguzi uliofanywa na Jumuiya ya maradhi yasiyoambukiza Zanzibar (Z NCDA) katika siku ya afya ya Tamasha la Vyakula vya Asili lililofanyika Makunduchi mwaka jana, alisema asilimia 24 ya watu waliofanyiwa uchunguzi waligundulika kuwa na sinikizo la damu na asilimia 4.3 walikuwa na maradhi ya sukari.
Hata hivyo alisema zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wanauelewa juu ya maradhi yasiyoambukiza na umuhimu wa kufanya mazoezi katika kujikinga na maradhi hayo.
Omar aliwasisitiza wananchi kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi na kutumia matunda kwa wingi kwani imebainika baadhi ya watu hawajui umuhimu wa matunda katika kupambana na maradhi yasiyoambukiza.
CAPTIONS
Picha No.01- Mratibu wa Jumuiya ya maradhi yasiyoambukiza Zanzibar (Z-NCDA) Haji Khamis akitoa tarifa ya mradi mpya wa afya kwa wanafunzi wa skuli za Sekondari za Wilaya ya Mjini Unguja.
Picha No.02- Baadhi ya wandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakifuatilia mkutano wa Z-NCDA uliofanyika ofisi ya Jumuiya hiyo Mpendae.
Picha No.03- Kaimu Meneja wa Kitengo cha maradhi yasiyoambukiza Wizara ya Afya Zanzibar Omar Abdallah Ali (kulia) Mwenyekiti wa Z-NCD Said gharib Bilal akitoa tarifa ya uchunguzi wa maradhi yasiyoambukiza katika Tamasha la vyakula vya asili lilifanyika Makunduchi mwaka jana.
Picha No.04- Makamu mwenyeki wa Jumuiya ya maradhi yasiyoambukiza Zanzibar Ali Zubeir Juma akitoa ufafanuzi wa maswali ya wandishi wa habari (hawapo pichani).
Picha na Makame Mshenga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.