Habari za Punde

NMB Yakutana na Wanachama wa Bussines Club Zanzibar na Kukabidhi Vyeti kwa Wajasiriamali Waliopata Mafanikio Kupitia Bussines Club Zanzibar

Naibu Waziri wa Ujenzui Mawasiliani na Usafirisha Zanzibar Mhe. Mohammed Ahmad akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Wajasiriamali na Wafanyabiashara Zanzibar zaidi wa 300 kupitia Business Club Zanzibar NMB uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madina Zanzibar, kuzungumzia ushuhuda na mafanikio ya Biashara zao kupitia Business Club NMB Zanzibar.
Mwenyekiti wa NMB Bussines Club ya Zanzibar,Ndg.Charunga Ali Madabida akifunga mkutano wa NMB Business Club Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madina Mazizini Zanzibar na kuwashirikisha Wafanyabiashara na Wajasiriamali zaid ya 300, kushoto Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ndg. Omar Ali Bhai na kulia Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara NMB Ndg. Donatus Richard.
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Zanzibar Ndg.Abdallah Duchi, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya Mkutano na Wafanyabiashara na Wajasiriamali wa NMB Business Club Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madina Mazizini Zanzibar.
Mkurugenzi Kitengo cha Biasha NMB Ndg. Donatus Richard kulia akimakabidhi Shuhuda wa Mafanikio ya Biashara kupitia NMB Bussiness Club Zanzibar Mjasiriamali wa Catalunia Barber Shops (ZANGA) Ndg. Hassan Ali, wakati wa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madina Mazizini Zanzibar.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya NMB Tanzania Ndg.Donatus Richard akizungumza wakati wa Mkutano na Wajasiriamali na Wafanyabiasha wa Bussiness Club uliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Madina Mazizini Zanzibar.
Mwenyekiti wa NMB Zanzibar Bussines Club,Ndg. Charunga Ali Madabida (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ndg.Omar Ali Omar Bhai., wakati wa hafla ya Mkutano wa Bussines Club wa NMB uliofanyika katika ukumbi wa mkutano wa Hoteli ya Madina Mazizini Zanzibar. 
Mjasiriamali Bi.Maureen Andrew wa Maia Bay akielezea mafanikio aliyoyapata kubitia Bussines Club NMB , wakati wa mkutano huo uliowakutanisha Wajasiriamali na Wafanyabiashara wa Zanzibar kuzungumzia changamoto zao na mafanikio wa;liopata kupitia NMB, Bussines Club.
Mkurugenzi wa Muna Beauty Academy Bi. Munawar Mbarouk , akizungumza wakati wa mkutano huo wa Bussines Club kupitia NMB, mafanikio yake aliyoyakapa kupitia NMB Bank katika mradi wake, akitowa ushuhuda huo wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madina Mazizini Zanzibar.
Mgeni Rasmin wa Mkutano wa Wajasiriamali na Wafanyabiasha Zanzibar wa Bussines Club NMBNaibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe.Mohammed Ahmad akimkabidhi Cheti kwa shuhuda wa Ujasiriamali wa Kampuni ya Yassers Laundry Ndg Mrisho Haji Mrisho, wakati wa mkutano huo wa Bussines Club NMB uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madina Mazizini Zanzibar.
Naibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe. Mohammed Ahmada akinunua bidha za Wajasiriamali kupitia Mkutano wa Bussines Club Zanzibar, uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Madina Mazizini Zanzibar, kushoto Meneja wa NMB Tawi la Zanzibar Ndg. Duchi.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.