Habari za Punde

Bonanza la Mchezo wa Pasaka Kati ya ZSSF na NSSF Uwanja wa Mao Zedung's Zanzibar Timu ya NSSF Yaibuka Mshindi wa Bonaza hilo Kwa Mikwaju ya Penenti 8-7 Baada ya Kutoka Droo Bila ya Kufungana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF Bi. Sabra Issa Machano akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Mchezo wa Bonaza la Pasaka Nahodha wa Timu ya NSSF Abubakar Sadiq baada ya kuibuka mshindi wa Bonaza hilo la Pasala lililofanyika Uwanja wa Mao Zedungs Zanzibar leo, Timu hiyo imeshinda kwa Mikwaju ya Penenti 8-7, katika ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Willian Erio.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Ndg. Willian Erio akikabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Michezo ya Bonaza la Pasaka na Nahodha wa Timu yake Abubakar Sadiq, baada ya kuifunga Timu ya ZSSN kwa mabao 8-7 kwa mikwaju ya penenti mchezo uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung's leo ikiwa ni shamrashamra ya michezo ya Pasaka mwaka huu yamefanyika Zanzibar.
Mchezaji wa Timu ya NSSF akimiliki mpira huku mchezaji wa Timu ZSSF akijaribu kumzuiya wakati wa mchezo wa Bonaza la Pasaka uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung's leo kuadhimisha michezo ya Pasaka iliofanyika kwa mwaka huu kisiwani Zanzibar kushirikisha wanamichezo kutoka Tanzania Bara na Visiwani.Timu ya NSSF imeshinda kwa mikwaju ya penenti 8-7.
Mchezaji wa Timu ya ZSSF akimpita beki wa Timu ya NSSF wakati wa mchezo wao wa Bonaza la Pasaka lililofanyika katika Uwanja wa Mao Zedung's leo. 
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Ndg. Willian Erio na Mkurugenzi Mkuu wa ZSSF Bi. Sabra Issa Machano mwenye miwani wakifuatilia mchezo huo wa Timu zao kusherehekea Pasaka uliofanyika Uwanja wa Mao Zedung's leo Timu ya NSSF imeshinda kwa bao 8-7. Kwa penenti baada ya kutoka sare ya bao 1-1.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.