Habari za Punde

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM CHAADHIMISHA WIKI YA UTAFITI KATIKA KITIVO CHA IMS BUYU ZANZIBAR

 Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Zanzibar Dkt. Omar Ali Khamis akifurahiya kitu alipokuwa akitoa hutuba kwenye maadhimisho ya Wiki ya Utafiti ya Chuo Kikuu cha Dar es salaa Kampasi ya Buyu Wilaya ya Magharibi B Unguja.
 Mkurugenzi Tasisi ya Sayansi za Bahari Zanzibar Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Margareth Serapio akizungumza katika maadhimisho ya tano ya Wiki ya Utafiti yaliyofanyika Kampasi ya Buyu, nje kidogo ya Mji wa Zanzibar, (kulia) Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Zanzibar Dkt. Omar Ali Khamis.
Baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Sayansi za Bahari, na wanafunzi wa shahada ya uzamili wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Zanzibar Dkt. Omar Ali Khamis (hayupo) alipokuwa akiwahutubia katika maadhimisho ya Wiki ya Utafiti.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kampasi ya Buyu Zanzibar akiwafahamisha kitu wanafunzi wa Skuli ya sekondari ya Lumumba walipotembelea chumba cha utafiti huko Buyu katika sherehe za Wiki ya Utafiti.
Mgeni Rasmi (katikati) katika picha ya pamoja na viongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na wanafunzi wa skuli ya Lumumba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.