Habari za Punde

KVZ Yajiandaa Kishinda Kila Mchezo Wao Ligi Kuu ya Zanzibar.


Na Hawa  Ally
KOCHA wa timu ya soka ya KVZ Sheha Khamis amesema kuwa wanajiandaa kushinda kila mechi ili kujiweka katika mazingira mazuri lakini ubingwa ni majaaliwa ya Mungu.

Khamis aliyasema hayo juzi mara baada ya kumalizika kwa mchezo kati yake na timu ya JKU uliochezwa Mao ambapo timu hiyo ilishinda kwa jumla ya mabao 2-0.

Alisema kuwa yeye kuhusu ubingwa hawezi kuuzungumzia kabisa kutokana na kwamba hayo ni majaaliwa yake mungu lakini kazi kubwa ambayo huifanya ni kuwahamasisha wachezaji wake wacheze vizuri ili kuweza kushinda.

“Kazi kubwa ninayoifanya ni kujiandaa ili tuweze kushinda na sio kujihakikishia kuwa bingwa kwa vile haya ni majaaliwa ya mungu”, alisema.

Hata hivyo alisema kuwa anashukuru kuona viongozi wa timu hiyo wanamsikiliza na kumpa ushirikiano hasa kwa ajili ya mechi hiyo ambayo ilikuwa ngumu kwa upande wake.

Hivyo alisema kuwa ni imani yake kwamba ushirikiano huo ukiendelea na timu yake itazidi kuwa na maendeleo mazuri zaidi hasa katika ligi hiyo ambayo kwa sasa ipo katika hali ngumu.

KVZ ipo nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 70 wakati JKU inashika nafasi ya pili kwa pointi 67 na Zimamoto ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 66.

    

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.