Habari za Punde

Mkutano wa Wakulima wa Zao la Karafuu Kisiwani Pemba

Mdhamini wa ZSTC Pemba, Abdalla Ali Ussi, akieleza jambo kwa wakulima wa Zao la Karafuu wa Wilaya ya Micheweni Pemba , katika Mkutano wa Wakulima hao uliotayarisha na shirika hilo huko katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni Pemba.
Mjumbe wa Bodi  ya Wazalishaji Karafuu Zanzibar, Maalim Mohammed Anadi Mohammed, akifunguwa Mkutano wa Wakulima wa Zao  la Karafuu huko katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni Pemba, uliotayarishwa na shirika la ZSTC.
Baadhi ya Wakulima wa Zao la Karafuu Wilaya ya Micheweni Pemba ,wakimskiliza Mjumbe wa Bodi ya Wazalishaji Karafuu Zanzibar, Maalim Mohammed Anadi Muhammed, wakati akifunguwa mkutano wa Wakulima hao huko katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo uliko Micheweni Pemba.
Kitambulisho cha mkulima  wa  Mikarafuu kilivyo , ambacho hutolewa na ZSTC baada ya kumalizika zoezi la usajili wa mkulima husika.
(Picha na Bakari Mussa -Pemba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.