Habari za Punde

Taasisi ya Samail Academy Kisiwani Pemba Yafutarisha Watoto Wenye Mazingira Magumu Kisiwani Pemba.

Waumini wa Dini ya Kiislam Kisiwani Pemba wakishiriki katika Sala ya Magharibi wakati wa hafla ya Futari ilioandaliwa na Taasisi ya Samail Academy ya Chakechake Pemba kwa Watoto wenye mazingira magumu iliofanyika katika ukumbi wa Taasisi hiyo Gombani.
MKURUGENZI wa Taasisi ya Samail Academy Nassir bin Said,wa kwanza kutoka kushoto akiwaongoza wananchi mbali mbali katika futari maalumu iliyoandaliwa na taasisi yake, huko katika viwanja vya Gombani
AFISA Mdhamini Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Fatma Hamad Rajab, wakanza kulia akiwaongoza wananchi na walezi wa watoto mayatima katika futali maalumu iliyoandaliwa na taasisi ya Samail Academy iliyopo Chake Chake
BAADHI ya watoto mayatima waliopo chini ya taasisi ya Samail Academy Kisiwani Pemba, wakipata futari maalumu iliyoandaliwa na taasisi hiyo huko Gombani Chake Chake Pemba
AFISA Mdhamini Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Pemba Fatma Hamad Rajab, akitoa neneo la shukuran kwa wananchi mbali mbali waliohudhuria futari maalumu na kufanyika katika viwanja vya Gombani
(Picha na Abdi Suleiman - Pemba)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.