Habari za Punde

Mashindano ya kumuenzi Marehemu Hassan Gharib yazinduliwa



Mwakilishi wa Jimbo la Dimani Dkt. Mwinyihaji Makame Mwadini akikaguwa timu katika ufunguzi wa mashindano ya Hassan Gharib CUP bweleo mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, alliempa mkono ni mchezaji wa timu ya Mitondooni Khamis Ali. Picha na Mwajuma Juma

NA MWAJUMA JUMA

MWAKILISHI wa Jimbo la Dimani Dkt. Mwinyihaji Makame Mwadini amezinduwa rasmi mashindano ya pili ya  kumuenzi Marehemu Hassan Gharib.

Mashindano hayo yatafanyika katika uwanja wa Bweleo ambapo Mwakilishi huyo aliwataka wachezaji wa timu shiriki kucheza kwa amani na utulivu ili kuendeleza kwa vitendo matendo ya marehemu.

Alisema kuwa wanafanya mashindano hayo kwa lengo la kumuenzi marehemu Hassan Gharib ambae alikuwa mdau mkubwa wa mpira pamoja.na kupenda amani na utulivu.

Hivyo wanachokitaka wao ni kuona mashindano hayo yanatumika kwa kuonesha vipaji na soka la upinzani litakalovutia watazamaji.

Mapema akisoma risala Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano hayo Said Majid alisema kuwa changamoto kubwa iliyopo ni vilabu kuomba kuongezewa kwa zawadi ili ziweze kulingana na zawadi za mashindano mengine ya ndondo, ambayo hapa Zanzibar ili kuzidi hamasa na timu nyengine zaidi zizidi kushiriki.

Michuano hiyo inashirikisha timu 16 yana lengo la kulienzi jina la kaka yao marehemu Hassan Gharib ambae alikuwa ni miongoni mwa wanabweleo amabao ni muhimili mkubwa wa timu hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.