Habari za Punde

Mchanga unapokuwa Dili


Kuadimika kwa mchanga katika mji wa Zanzibar kumepelekea baadhi ya wananchi kutafuta njia mbadala ya kujipatia mchanga ili kuweza kuendeleza ujenzi.

Camera ya Zanzinews iliwanasa wananchi hawa katika mitaa ya Kisimamajongoo mjini Zanzibar wakiwa busy kusafisha mitaro ya maji, si kwa ajili ya usafi bali kwa ajili ya kujipatia mchanga ambao nilipowauliza walisema wanauza kila Polo Sh 2000/= na kila siku hupata zaidi ya Polo 20.

Wafanyakazi wa Manispaa hamna budi kuwashukuru wasamaria hawa wema kwa kuwapunguzia mzigo wa kazi za kusafisha mitaro.

Kweli mjini ni Shule

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.