Habari za Punde

Meneja Kiongozi wa Uhusiano wa PSSSF Bi. Eunice Chiume Atembelea Vyombo Vya Habari Jijini Dar es Salaam.

Bi. Eunice Chiume akizungumza katika kutano huo wa pamoja na uongozi wa gazeti la Nipashe na The Guardian.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MENEJA Kiongozi Uhusiano, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi.Eunice Chiume, amefanya ziara ya kutembelea vyombo vya habari vinne jijini Dar es Salaam leo Juni 10, 2019 kwa lengo la kueleza shughuli za Mfuko huo ikiwa ni pamoja na kujenga mahusiano mema ya ushirikiano baina ya Mfuno na tasnia ya habari.
Katika ziara hiyo iliyoanzia kwenye ofisi za The Guardian Limited Mikocheni jijini Dar es Salaam, Bi. Eunice alifuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi ambapo walipokelewa na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe, Bi. Beatrice Bandawe na kisha baadaye kufanya mazungumzo yaliyowahusisha, pia Mhariri Mtendaji wa The Guardian, Bw. Wallace Mauggo na wahariri wengine.
Baada ya kutembelea The Guardian, ziara ya Bi. Eunice ilimfikisha pia kwenye ofisi za Global Group zinazomiliki vyombo vya habari vya kielekrtorniki na magazeti, na kisha kumaliza ziara yake kwenye ofisi za EML na EFM Radio.
Akizungumza kwa nyakazi tofauti kwenye ofisi za vyombo hivyo, Meneja huyo alisema, nia ya ziara hiyo ni kueleza shughuli za Mfuko huo ambao ni matokeo ya kuunganishwa mifuko mine ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF.
“Lakini niseme tu kwamba vyombo vya habari ni wadau wakubwa katika kuhakikisha Umma wa watanzania unapata habari na taarifa mbalimbali zinazohusu Mfuko huu mpya wa PSSSF kwa hivyo tumeona ni muhimu kuwatembelea ili kubadilishana mawazo na kujenga mahusiano mema ya kiutendaji.” Alsiema Meneja huyo Kiongozi.
Alisema, PSSSF ilianza rasmi kutekeleza majukumu yake tarehe 1 Agosti, 2018, hivyo bado ni Mfuko mpya ambapo wanachama na wastaafu wa Mfuko huu wanalazimika kujua sheria mpya zinazoendesha Mfuko na watu pekee wanaoweza kufikisha elimu hiyo kwa haraka ni vyombo vya habari.
“Kwa sasa nitoe wito tu kwa wastaafu wote kwenda kwenye ofisi zetu zilizoenea nchi nzima bara na visiwani ili kuhakiki taarifa zao kwani zoezi hilo ni muhimu na linaendelea.” Alisema.
 Meneja Kiongozi Uhusiano, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Ummae (PSSSF), Bi.Eunice Chiume, (watatu kushoto), Afisa Uhsiano mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, (wakwanza kushoto), wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe, Bi. Beatrice Bandawe (wane kushoto), Mwandishi Mkuu wa gazeti hilo, Bi. Salome Kitomari (watano kushoto), Mhariri msanifu, Deodatus Muchunguzi (wakwanza kulia) na mkuu wa kitengo cha digitali cha gazeti hilo, muda mfupi baada ya Meneja huyo kutembelea chumba cha habari cha The Guardian katuka ziara ya kutambulisha Mfuko huo mpya kwa vyombo vya habari nchini. Ziara hiyo imefanyika leo Juni 10, 2019.akizungumza na uongozi wa gazeti la Nipashe, chini ya Mhariri 
  Meneja Kiongozi Uhusiano, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Ummae (PSSSF), Bi.Eunice Chiume, (kushoto), akizungumza na uongozi wa gazeti la Nipashe, chini ya Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo, Bi.Beatrice Bandawe, (watatu kushoto) alipotembelea chumba cha habari cha gazeti hilo jijini Dar es Salaam leo Juni 10, 2019. Bi.Chiume ameanza ziara ya kutembelea vyombo vya habari ili kueleza shughuli za Mfuko huo mpya ikiwa ni pamoja na kukuza ushirikiano
 Meneja Kiongozi uhusiano Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Ummae(PSSSF), Bi.Eunice Chiume, (wapili kushoto, akiwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko hio, Bw.Abdul Njaidi, (kushoto), akizungumza na uongozi wa gazeti la Nipashe, chini ya Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo, Bi.Beatrice Bandawe, (watatu kushoto) alipotembelea chumba cha habari cha gazeti hilo jijini Dar es Salaam leo Juni 10, 2019. Bi.Chiume ameanza ziara ya kutembelea vyombo vya habari ili kueleza shughuli za Mfuko huo mpya ikiwa ni pamoja na kukuza ushirikiano. 
 Mhariri Mtendajiw a gazeti la The Guardian, Bw. Wallace Mauggo, (kushoto), akizunguzma na Meneja Kiongozi uhusiano, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Ummae(PSSSF), Bi.Eunice Chiume kwenye chumba cha habari cha The Guardian jijini Dar es Salaam Juni 10, 2019.
 Bi. Eunice akisindikizwa na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe, Bi. Beatrice Bandawe mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea chumba cha habari cha The Guardian. Wengine ni Afusa Uhusiano Mwandamizi wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi (kulia) na Mwandishi Mkuu wa Nipashe, Bi. Salome Kitomari.
 Meneja wa kampuni ya Global Group, Bw. Abdallah Mrisho (kulia), akimpa maelezo Meneja Kiongozi Uhusiano Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi.Eunice Chiume, (wapili kushoto, akiwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko hio, Bw. Abdul Njaidi, (watatu kushoto) wakati alipotembelea chumba cha habari cha Global Publishers, Sinza jijini Dar es Salaam Juni 10, 2019. Wakwanza kushoto ni Mhariri Mytendaji wa magazeti yanayomilikiwa na kampuni hiyo, Bw. Saleh Ally.
 Bi. Eunice Chiume, (watatu kushoto) akiwa na Bw. Abdul Njaidi (kulia), wakiongozwa na wenyeji wao, Meneja wa Global Publishers, Bw. Abdallah Mrisho (wakwanza kushoto) na Bw. Salehe Ally wakati alipote,mbelea ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, Juni 10, 2019.
 Mwenyekiti na Afisa Mtednaji Mkuu wa Global Group, Bw. Eric Shigongo (kushoto), akimsikizia Meneja Kiongozi Uhusiano, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi.Eunice Chiume wakati alipotembelea vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam Juni 10, 2019.
 Bi. Eunice Chiumew akiwa kwenye studio za Global Radio
 Mkurugenzi Mtendaji wa EML na EFM Radio Bw.Francis Anthony Ciza akisalimiana na Meneja Kiongozi Uhusiano PSSSF Bi. Eunice Chiume wakati alipotembela ofisi za vyombo vya habari vinavyomilikiwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam Juni 10, 2019
Bi. Eunice Chiume akipokelewa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa  EFM Radio, Bw.Dennis Busulwa (Ssebo) wakati alipotembelea ofisi za Radio hiyo jijini Dar es Salaam Juni 10, 2019.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.