Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Ahudhuria Hitma na Kuifariji Familia ya Dr. Badria Abubakar Gurnah

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na kumpa mkono wa Pole Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi alipofika nyumbani kwao Mikocheni Jijini Dar es Salaam kuifariji familia ya Dr. Badria Abubakar Gurnah.
Rais wa Zanzibar nma Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwafariji Watoto wa Marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah alipofika nyumbani kwao Mikocheni Jijini Dar es Salaam kutowa mkono wa pole na kuwafariji kwa kuondokewa na mpendwa Mama yao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akisaini kitabu cha maombelezi alipofika nyumbani kwa marehemu Badria Abubakar Gurnah Mikocheni Jijini Dar es Salaam, kushoto Mama Mwanamwema Shein.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akisaini kitabu cha maombolezi cha Dr. Badria Abubakar Gurnah, alipofika nyumbani kwa marehemu kuifariji familia na kutowa mkono wa pole. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akimfariji Mtoto wa Marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah, Zaina Abdalla Juma Mabodi kulia Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi. alipofika nyumbani kwao kutowa mkono wa pole na kuifariji familia
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dk. Ali Mohamed Shein kulia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi, wakitowa mkono wa pole na kuifariji familia ya marehemu alipofika nyumbani kwao Mikocheni Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dr. Ali Mohamed Shein, na kulia Mma Mwanamwema Shein kushoto Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi na Wanafamilia.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kushoto Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na kulia Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi wakijumuika na Wanafamilia na Wananchi katika hitma ya kumuombea Marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah iliofanyika nyumbani kwao Mikocheni Jijini Dar es Salaam.
Wananchi wa Jijini Dar es Salaam wakijumuika na Familia ya Marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah iliofanyika nyumbani kwao Mikochezi Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuika na Wananchi katika kisomo cha hitma marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah iliofanyika nyumbani kwao Mikocheni Jijini Dar es Salaam.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akipiga fatha kabla ya kuaza kwa kisoma cha dua na hitma ya kumsomea Marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah, iliofanyika katika Masjid Mahamur  Upanga Jijini Dar es Salaam, kulia Mume wa Marehemu Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdalla.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dr. Ali Mohamed Shein, akiongoza kisomo cha Hitma ya Marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah kilichofanyika katika Masjid Mahamur Upanga Jijini Dar es Salaam kulia Mume wa Marehemu Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi na kushoto Sheikh Ayoub Ali Seif na Sheikh Zeni Shariff.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakishiriki katika kisomo cha Hitma ya Marehemu Dr. Badria Abubakar Gurnah kilichofanyika katika Masjid Mahmamr Upanga Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiitikia dua baada ya kumalizika kisomo cha hitma ya Dr. Badria Abubakar Gurnah, kulia Mume wa Marehemu Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dr. Abdalla Juma Mabodi na kushoto Sheikh Ayoub Ali Seif na Sheikh Zeni Shariif akisoma dua hiyo.
Mjomba wa Marehemu Dr. Badria akitowa neno la shukrani kwa niaba ya familia kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein na Wananchi wote waliohudhuria kisomo cha hitma ya marehemu Mtoto wao Dr. Badria Abubakar Gurnah, kilichofanyika katika Masjid Mahamur Upanga Jijini Dar es Salaam.kilichofanyika jana usiku.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.