Habari za Punde

Wadi ya Kianga wahitimu darasa la Itikadi

na Takdir Suweid, Wilaya ya Magharibi 
Vijana wametakiwa kujiunga na Madarasa ya itikadi ili kujuwa historia ya nchi yao na kuepuka na kupotoshwa Mitaani.
Wito huo umetolewa huko Kianga na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Magharibi Bw. Mgeni Mussa Haji wakati alipokuwa akifunga mafunzo ya elimu ya Darasa la Itikadi kwa Vijana 80 wa Wadi ya Kianga Wilaya ya Magharibi A.
Amesema baadhi ya Watu wanawapotosha Vijana juu ya Historia ya Nchi yao hivyo iwapo watajiunga na Madarasa hayo wataweza kuwa Wazalendo wa kulinda Taifa lao.
Amesema matarajio ya kutoa elimu hiyo ni kuzidi kukipatia ushindi Chama hicho katika Uchaguzi uchaguzi Mkuu ifikapo 2020.
Akielezea kuhusu Tatizo la Ajira kwa Vijana Bw.Mgeni amewataka kujiunga katika Vikundi ili kuweza kupatiwa Mitaji itakayowawezesha kujiajiri wenyewe na kuepukana na kutegemea Serikalini  pekee kwani Idadi ya Vijana wanaohitaji ajira ni kubwa ukilinganisha na nafasi zilizopo.
Akisoma risala katika hafla hiyo Ali Kelvin Kitwana ameomba kupatiwa ufumbuzi matatizo ya Ajira na kumalizia ujenzi wa choo cha Tawi la ccm Muembemsala ili kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Nao Wahitimu hao wameahidi kuifikisha elimu hiyo kwa wenzao na kuiomba Serikali kuondoshea matatizo yanayowakabili ikiwemo ukosefu wa Ajira ili kuweza kujikinga kujiingiza katika Vikundi viovu kutokana na tatizo la ukosefu wa Ajira.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.