Habari za Punde

Wafanyakazi wa  Ofisi ya Makamu wa Rais katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma leo imefanya usafi katika eneo la Makulu jijini Dodoma kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji, NEMC, Wadau mbali mbali wa mazingira pamoja na Wananchi wa Makulu.
Wakazi wa Makulu jijini Dodoma wakiwa na vifaa vyao vya usafi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine (hayupo pichani) kabla ya kuanza kwa zoezi la usafi lililoratibiwa na Ofisi yake ikiwa Sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma

Wananchi na Wadau wa Mazingira wakishiriki zoezi la usafi katika eneo la Makulu, Dodoma ambapo taka za mifuko ya plastiki zilipewa kipaumbele, zoezi hili liliandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi  Umma. 
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Patrobas Katambi akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali, Wadau wa mazingira na Wananchi mara baada ya kumaliza zoezi la usafi katika eneo la Makulu Dodoma, zoezi hilo liliratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dodoma ikiwa sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma.

 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine (mwenye kofia) akiongoza watumishi wa ofisi yake pamoja na wananchi wa Makulu, Dodoma kufanya usafi ikiwa sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.