Habari za Punde

Mafunzo ya Wiki Moja ya Walimu wa Makipa Zanzibar.

Na.Mwanajuma Juma.
WALIMU wa soka visiwani Zanzibar wametakiwa kuwa na ushirikiano ili kujenga mustakbali mwema wa soka la Zanzibar.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Soka ZFA wilaya ya Mjini Hassan Haji Hamza katika ufungaji wa Mafunzo ya siku sita ya waalimu wa makipa yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Zanzibar ZFF na kufanyika uwanja wa Amaan mjini hapa.

Alisema kuwa kumejengeka tabia ya waalimu kutopendana jambo ambalo linaufanya mpira wao kudorora.

"Nimefanya utafiti na kubaini kitu kimoja sana kibaya nacho ni kwamba waalimu wa soka Zanzibar Wana roho mbaya Sana, maisha amepanga mungu hata ufanye nini huwezi kumshusha", alisema.

Alifahamisha kwamba kuna watu wanakuwa  hawajui kitu na wanajuwa Kuna mtu anajua lakini anashindwa kumfata na kupelekea kuharibu kwa makusudi.

"Tabia hii sio nzuri kwa kweli na kwa vile tunataka mafanikio ni lazima tushirikiane, wacheni hili kuweni na mashirikiano penye mafanikio utaonekana tu", alisema.

Alieleza kuwa suala hilo linafanyika kutokana na watu kutokuwa na uyakini kwa mwenziwe na badala yake watakuwa wanazungumza vizuri lakini kumbe rohoni mwake kuna choyo.

Mapema katika risala yao iliyosomwa na Abdilahi Silima waliiomba ZFF Kusimamia kikamilifu kanuni iliyopangwa juu ya kuwatumia waalimu waliosoma ili waweze kunufaika na elimu waliyoipata.

Aidha waliiomba ZFF kuhakikisha wanatoa vitambulisho maalumu vya kuingilia uwanjani ili kuepusha usumbufu wa uingiaji wa uwanjani.

Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo Saleh Ahmed Machupa alisema kuwa amefarijika Sana na mahudhurio ya waanafunzi hao na kukivunia kwa kutofeli hata mmoja.

Mafunzo hayo ya siku sita yalishirikisha waalimu 26, wakiwemo Wanawake watano na.wanaume 21 ambao Ni kutoka Zanzibar na Tanzania bara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.