Habari za Punde

Michuano ya Kipwida Yatowa Burudani Kwa Wanamichezo Zanzibar.

TIMU ya soka ya Usipagawe ya Uzi juzi imeendelea kupokea kichapo katika michuano ya Kombe la kipwida kwa kufungwa na White Stone bao 1-0.

Mchezo huo ambao ni mwendelezo wa michuano hiyo inayochezwa kwenye uwanja wa Maungani ni wa pili kwa kwa timu hiyo kuupoteza.

Katika mchezo huo bao la pekee la timu hiyo ya White Stone nayo ni mechi yake ya pili kushinda kufatia mechi ya kwanza kufungwa mabao Tola Combine mabao 2-0 lilifungwa na Mohammed Zimbwe.

Ushindi wa timu hiyo bado unaliweka katika wakati mgumu kundi hilo ambapo mpaka Sasa timu ya Tola pekee ndio inayoonesha mazingira mazuri ya kuingia hatua ya robo fainali.

Leo kutakuwa na mchezo Kati ya timu ya Sarayevo Home Boys na timu ya Mafriji Fc.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.