Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi Azungumza na Madaktari Bingwa Kutoka Chuo Kikuu Cha Alexandria Nchini Misri.

Kiongozi wa Timu ya Madaktari Mabingwa wa Chuo Kikuu cha Alexadria Nchini Misri Profesa Sabri Wahid akielezea malengo ya kuweka Kambi Zanzibar kwa ajili ya kusaidia huduma za Afya.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kati kati akizungumza na Timu ya Madaktari Mabingwa wa Chuo Kikuu cha Alexadria Nchini Misri ukiwa Zanzibar kuweka Kambi kwa ajili ya upasuaji wa Wagonjwa waliozaliwa na Maradhi yasiyo ya kawaida.
Balozi Seif kulia akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake ya Timu ya Madaktari Mabingwa kutoka Chuo Kikuu cha Alexadria Nchini Misri.Kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Afya Zanzibar Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed.
Kiongozi wa Timu ya Madaktari Mabingwa wa Chuo Kikuu cha Alexadria Nchini Misri Profesa Sabri Wahid akimkabidhi zawadi Maalum Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya Mazungumzo yao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimkabidhi zawadi za biadhaa za Viungo Kiongozi wa Timu ya Madaktari Mabingwa wa Chuo Kikuu cha Alexadria Nchini Misri Profesa Sabri Wahid mara baada ya Mazungumzo yao.
Balozi Seif aliyevaa koti na Kanzu kati kati akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Madaktari Mabingwa wa Chuo Kikuu cha Alexadria Nchini Misri pamoja na Uongozi wa Wizara ya Afya Zanzibar mara baada ya mazungumzo yao.
Picha na –OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema msaada mkubwa unaoendelea kutolewa na Madaktari Mabingwa wa Afya kutoka Chuo Kikuu cha Alexandria Nchini Misri unazidi kuleta faraja kwa Wananchi waliowengi Visiwani Zanzibar.
Alisema Familia kadhaa zilizowahi na zinazoendelea kupata huduma za Upasuaji kwa Wagonjwa wao kupitia Madaktari Mabingwa hao wa Misri wanaokuja Zanzibar kwa vipindi tofauti tokea Mwaka 2013 zimejenga matumaini makubwa ya kuimarika kwa Afya za Wagonjwa wao.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati akizungumza na Timu ya Madaktari Mabingwa  kutoka Chuo Kikuu cha Alexandria Nchini Misri waliowasili Zanzibar kufanya upasuaji kwa Wagonjwa 66 waliozaliwa na Maradhi yasiyo ya kawaida.
Alisema ujio wa Timu hiyo ya Wataalamu wa Afya kwa upande mwengine mbali ya kutoa huduma za Afya lakini pia utaongeza fursa za Utaalamu kwa Madaktari Wazalendo waliopo hapa Nchini.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushauri na kuuomba Uongozi wa Chuo Kikuu cha Alexandria kuendelea kutoa nafasi zaidi za mafunzo ya juu kwa Madaktari Wazalendo wa Zanzibar kwenye Vyuo Vikuu mbali mbali Nchini Misri Taifa ambalo limepiga hatua kubwa katika Taaluma ya Afya.
Mapema Kiongozi wa Timu ya Madaktari Mabingwa wa Afya kutoka Chuo Kikuu cha Alexandria Nchini Misri Profesa Sabri Wahid alisema operesheni 350 tayari zimeshafanyika kupitia mfumo huo wa uwekaji Kambi ikiwa ni mara ya Sita tokea ulipoanzishwa mnamo Mwaka 2013.
Profesa Sabri alisema operesheni za Kambi ya Mwaka huu zinahusisha Watoto wapatao 52 na Watu Wazima 14 waliozaliwa na  matatizo yasiyo ya kawaida katika maumbile ya Mwanaadamu.
Alisema uamuzi wa Uongozi wa Chuo hicho wa kuweka Kambi umekuja katika azma ya kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kupunguza gharama kubwa za Matibabu ambazo zingeigharimu Serikali katika kuwahudumia Wananchi wake.
Naye kwa upande wake Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Hamad Rashid Mohamed alisema Serikali kupitia Wizara anayoisimamia inaendelea kujenga Miundombinu imara katika Sekta ya Afya hasa Majengo kasi ambayo Misri ina fursa ya kuendelea kusaidia Utaalamu katika Sekta hiyo.
Mh. Hamad alisema Hospitali nyingi kubwa bado hazijatosheleza Watendaji wenye uwezo mkubwa unaolingana na Hospitali hizo zinazolenga kutoa huduma z Afya katika muda wote.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.