Habari za Punde

Ufunguzi wa Mkutano wa Tatu wa Vyuo Vikuu Vya Kiislam Duniani Yafanyika Zanzibar.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Simai Mohamed Said Kulia akimuongoza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kuelekea kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Manidat Al – Bahr kuufungua Mkutano wa Tatu wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu Duniani.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al – Simait Chukwani Profesa Amran Rasli akiwakaribisha Zanzibar Washiriki wa Mkutano wa Tatu wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu Duniani kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Manidat Al – Bahr Mbweni.
Mwakilishi wa Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia masuala ya Mtandao waMawasiliano ya Kiislamu {IIIT} Profesa Omar Kasule akielezea lengo la Taasisi yake katika kuimarisha Elimu ya Dini katika Mfumo wa Kisasa.
Mwakilishi wa Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia masuala ya Mtandao waMawasiliano ya Kiislamu {IIIT} Profesa Omar Kasule Kushoto na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al – Simait Chukwani Profesa Amran Rasli wakibadilishana hati za Mkata wa ushirikiano baada ya kutia saini mbele ya Mgeni rasmi Balozi Seif.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amnali Zanzibar Mh. Simai Mohammed Said akimkaribisha Balozi Seif  kuufungua Mkutano huo wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu Duniani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tatu wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu Duniani uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Manidat Al Bahr Mbweni Wilaya ya Magharibi "B" Unguja akimuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika Picha ya pamoja na Wahadhiri wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu vinavyoshiriki Mkutano wa Tatu wa Vyuo hivyo Shein hapo Hoteli ya Manidat Al – Bahr Mbweni.
Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.