Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko akimkabidhi zawadi aliyekuwa Mkurugenzi, Idara ya Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu Cleophas Ruhumbika, ambayo ni Picha yake aliyochorwa mstaafu huyo , wakati wa kumpongeza kwa kustaafu utumishi wake wa Umma leo, tarehe 21, Septemba, 2019.
Aliyekuwa Mkurugenzi, Idara ya Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu, Cleophas Ruhumbika, akionesha zawadi ya Picha yake iliyochorwa, mara baada ya kukabidhiwa wakati wa kumpongeza kwa kustaafu rasmi utumishi wake wa Umma leo
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu, Aristides Mbwasi, akilishwa keki na aliyekuwa Mkurugenzi Idara ya Uwekezaji , Cleophas Ruhumbika ambaye amestaafu, wakati wa kumpongeza kwa kustaafu utumishi wake wa Umma leo.
Baadhi ya Watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilila tukio la kumuuga rasmi aliyekuwa Mkurugenzi Idara ya Uwekezaji , Cleophas Ruhumbika ambaye amestaafu, wakati wa kumpongeza kwa kustaafu utumishi wake wa Umma rasmi, leo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Dorothy Mwaluko akieleza jinsi aliyekuwa Mkurugenzi, Idara ya Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu, Cleophas Ruhumbika, (kushoto kwake) anapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika kuchapa kazi kwa ufanisi na weledi, wakati wa kumpongeza kwa kustaafu rasmi utumishi wake wa Umma leo
Aliyekuwa Mkurugenzi Idara ya Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu, Cleophas Ruhumbika
ambaye amestaafu rasmi utumishi wake wa Umma leo, tarehe 21 Septemba, 2019, akieleza
jambo kwa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, wakati wa kumpongeza kwa kustaafu,
(kushoto kwake) ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu,
Aristides Mbwasi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu)Bi. Dorothy Mwaluko, akilishwa keki na aliyekuwa Mkurugenzi Idara ya Uwekezaji , Cleophas Ruhumbika ambaye amestaafu, wakati wa kumpongeza kwa kustaafu rasmi utumishi wake wa Umma leo, tarehe 21, Septemba, 2019
No comments:
Post a Comment