Habari za Punde

Makabidhiano ya Ofisi Baina ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na Wakusini Unguja leo.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud (Kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan wakitia saini ya makabidhiano katika Ofisi ya Mkoa wa Mjini Magharibi, hafla hiyo imefanyika ukumbi wa Ifisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjhini Magharibi Unguja Vuga leo.
Na  Mwashungi Tahir      Maelezo       23-9-2019.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud  amewataka wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi kuwa na mashirikiano mazuri katika uongozi mpya.
Ameyasema hayo leo huko katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi iliopo Vuga wakati wa makabidhiano ya hati za utendaji kazi ya Ofisi wa Mkuu wa Mkoa huo.
Amesema amepokea uteuzi kwa furaha na kuahidi atafanya kazi kwa jitihada kubwa kwani hayo ni maamuzi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein.
“Nimepokea kwa furaha na heshima zote na naahidi nitaendelea na majukumu yangu bila tatizo lolote kwani haya ni maamuzi ya Mh Rais wetu na mabadiliko ya kazi hutokea wakati wowote”alisema Ayoub.
Pia aliwashukuru wafanyakazi wa Mkoa huo kwa kufanya kazi  kwa mashirikiyano makubwa na kuwaomba na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi mpya wampe mashirikiano mazuri katika utendaji wake wa kazi.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan amesema anaahidi kuhakikisha Mkoa huo utaendelea kuwa na amani na utulivu na atahakikisha hakutotokea vitendo vya uvunjifu wa amani.
Aidha amesema atahakikisha usalama wa watalii utaendelea kuwepo kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama na wananchi nao wataendelea kuwa na aman ndanin ya Mkoa huo.
Amewaomba wafanyakazi hao kumpa mashirikiyano  kwa kuwa tayari kukubali  kukosolewa pale atapoonekana anakwenda kinyume na maadili ya kazi  .
“Niko tayari kushirikiyana na wasaidizi wangu na endapo nitapoonekana nakwenda kinyume na maadili ya kazi niko tayari kukosolewa “, alisema Mkuu wa Mkoa wa Mjini wa Magharibi.
Sambamba na hayo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Talib Ali Talib amesema atahakikisha kuwa na mashirikiyano na Mkuu huyo na kuhakikisha ufikapo uchaguzi mkuu 2020  Majimbo yote 22  yanashinda kwa kishindo.

Mshauri wa Waziri wa Habari,Utalii na Mambo ya Kale Abdallah Mwinyi akitoa nasaha kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan pamoja na Wafanyakazi wa Mkoa wa Mjini Magharibi katika utiaji wa saini ya makabidhiano  Ofisi ya Mkoa wa Mjini Magharibi Huko Vuga.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mjini Talib Ali Talib akiomba ushirikiano katika kazi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan wakati wa utiaji saini ya makabidhiano Ofisi ya Mkoa wa Mjini Magharibi Huko Vuga wakati Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan wa pili (kulia) wakibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Ayoub Mohamed Mahmoud.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mkoa wa Mjini Magharibi wakifatilia kwa makini utiaji wa saini ya makabidhiano Ofisi ya Mkoa wa Mjini Magharibi Huko Vuga.

Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.