Habari za Punde

Wanafunzi wa Kidatu Cha Sita Waliofanya Vizuri Mitihani Yao Wakabidhiwa Zawadi Kisiwani Pemba.

 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, akimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma kulia na Mfanyabiashara Maarufu Visiwani Zanzibar Ndg. Said Bopar na kushoto kwa Balozi ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Mhe. Simai Mohammed Said, wakiangalia moja ya Laptop iliotolewa zawadi kwa Wanafunzi wa Kidatu cha Sita waliofanya vizuri mitihani yao ya Taifa.
Balozi Seif akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Hassan Salum Abeid miongoni mwa wahitimu Bora wa Daraja la Kwanza kutoka Skuli ya Madungu zawadi ya Laptop pamoja na Mikoba.
Mwanafunzi Zulfa Khamis Omar wa Skuli ya Kiislamu akipokea zawadi ya Laptop, Mkoba na Bahasha Maalum kutoka kwa Balozi Seif zilizotolewa na Mfanyabiashara Said Bopar.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma akisisitiza umuhimu wa Washirika wa Sekta ya Elimu kuendelea kuunga mkono Fani hiyo kwenye hafla ya Kukabidhi zawadi kwa Wahitimu bora wa Daraja la Kwanza  Kidato cha Sita Kisiwani Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.