Habari za Punde

ZFF Yachanganyua Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar U-20.


Na. wanajuma Juma.
SHIRIKISHO la soka Zanzibar ZFF limesema kuwa linaendelea na mchakato wa kuchanganuwa wachezaji wa timu ya Timu ya Taifa ya Zanzibar U-20 itakayoshiriki michuano ya Chalenji nchini Uganda mwezi huu.

Hayo yamebainishwa na Katibu wa Shirikisho hilo Mohammed Hilal Tedy alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwao Amaan mjini hapa.

Alisema kuwa pamoja na kuwa timu hiyo inafanya mazoezi kwa ajili ya mashindano hayo na kusogeza mbele kukaa kambini hadi pale mchanganuo wao utakapokamilika.

Hata hivyo alisema kuwa pamoja na hilo lakini pia wanafanya uchunguzi wav yeti vya wachezaji kutokana na kuwa hawawezi kumpitisha mchezaji kambini hali ya kuwa hawajapata matokeo ya umri wake kupitia kwa Mrajisi wa vizazi na vifo .

Alisema kuwa wanafanya hivyo kwa sababu suala la umri wanatakiwa kuwa makini na ndio maana wamejikita kwenye upembuzi na kuhakikisha wanawapata wachezaji sahihi kiumri.

“Tumepeleka muda mbele wa kukaa kambi kutokana na kuendelea na mchanganuo wa wachezaji, tumefanya mazoezi lakini tunamchanganuo ili  kupata wachezaji waliosahihi”, alisema.

Hivyo aliongeza kwa kusema kuwa ili mchezaji aweze kuingia kambi ni lazima wapate orodha kutoka kwa Mrajisi kujuulikana kwamba anastahiki kumuweka kambini.

“Tuna dressing nzuri na vifaa vyote vipo kamili lakini tunaendelea na uchunguzi wa wachezaji na kuhakikisha tunawapeleka wachezaji wenye umri sahihi”, alisema.

Hata hivyo alisema kuwa tayari wamecheza mechi moja ya kirafiki ili kuweza kuitoa timu hiyo hadharani ili wananchi waweze kujuwa kama ipo
timu hiyo ya U-20 .

“Kwa ufupi ndio kwanza tunaanza ingawa tulianza taratibu ndefu lakini naamini hamasa itatokezea pale ambapo tutakapokuwa tushakamilika tutaweza kuitangaza timu vizuri, tutakaa vizuri, na sifikirii wazanzibari wakati tutakaposhiriki lakini kwenye maandalizi wanatizama kinaendelea nini lakini baadae wataipa sapoti”, alisema.

Timu hiyo ambayo ipo chini ya kocha Nassor Salum ‘Kocha Cholo’ ambae alitangazwa rasmi juzi kupewa jukumu la kuinoa timu hiyo ambayo itashiriki michuano ya Chalenji yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu nchini Uganda.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.