Habari za Punde

Hafla ya utiaji saini wa ujenzi wa Mahakama Tunguu

 Mtendaji Mkuu wa Mahkama Zanzibar Kai Bashir Mbaruk kulia akitiliana saini na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Advent Construction ltd Mkataba wa Ujenzi wa Mahkama Kuu Tunguu Mkoa Kusini Ungja. .hafla iliofanyika katika ukumbi wa Mahkama Kuu Vuga Zanzibar
  Mtendaji Mkuu wa Mahkama Zanzibar Kai Bashir Mbaruk kulia wakibadilishana hati ya  saini na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Advent Construction ltd Mkataba wa  Ujenzi wa Mahkama Kuu Tunguu Mkoa Kusini Ungja.hafla iliofanyika katika ukumbi wa Mahkama Kuu Vuga Zanzibar.
 Waziri wa Katiba na Sheria Khamis Juma Maalim akitoa hotuba katika hafla ya  utiliaji saini Mkataba wa  Ujenzi wa Mahkama Kuu Tunguu Mkoa Kusini Unguja.ambayo itakayojengwa na Kampuni ya Advent Construction ltd hafla iliofanyika katika ukumbi wa Mahkama Kuu Vuga Zanzibar.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu  akitoa hotuba katika hafla ya  utiliaji saini Mkataba wa  Ujenzi wa Mahkama Kuu Tunguu Mkoa Kusini Unguja.ambayo itakayojengwa na Kampuni ya Advent Construction ltd hafla iliofanyika katika ukumbi wa Mahkama Kuu Vuga Zanzibar.


PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Rahma Khamis na Mwashungi Tahir Maelezo.
          
  Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar  Khamis Juma Maalim ameitaka kampuni ya Advent Construction Limited kutoka Dar es Salaam  kukamilisha ujenzi wa Mahakama kuu Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja kujenga kwa muda waliokubaliana ambapo linatarajiwa kumalizika mwakani .
 Ameyasema hayo huko Mahakama Kuu Vuga wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  mara baada ya ghafla ya kutiliana saini na Kampuni ya Advent Construction ambayo inayotarajia kujenga Mahakama mpya Tunguu Mkoa wa Kusini  Unguja .
 Amesema kitendo cha kusaini mkataba huo ni muhimu sana  ikiwa  ni Utekelezaji wa  Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ikiwemo  kusimamia na kuimarisha haki  ili wananchi wapate haki za kusimamia kesi zao.
Amewataka  kujenga  jengo lenye ubora na kukamilisha  kwa muda uliopangwa ili wawe na jengo la kisasa na waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi  na kupata Mahkama iliyo nzuri Zanzibar ambapo inatarajiwa kumalizika hapo mwakani kabla ya Dkt Shein kumaliza uongozi wake ikiwa ni miongoni mwa  ahadi zake.

Pia amesema sheria ya msaada ishatungwa kwa lengo la kuandaa mazingira yaliyo mazuri kwa wananchi kupata haki zao kwa urahisi.
Hivyo amewaomba wakandarasi hao kujenga jengo lenye ubora  na kiwango madhubuti ili liweze kudumu kwa muda mrefu na kutarajia likimaliza litasaidia Serikali katika utendaji wake.
“Tunaomba jengo hili lijengwe kwa kiwango kilicho bora ili kuweza kudumu kwa muda mrefu na kuepuka kujenga jengo bila ya kiwango” alisema Waziri huyo.
Nae Jaji Mkuu Omar Othman Makungu amewataka wakandarasi hao kuhakikisha wanajenga Mahkama iliyo ya kupendeza ili na sie tuwe na Mahkama iliyo nzuri yenye sifa kwa Zanzibar na kufanya wafanyakazi kila kitendo kinapata sehemu ya kufanyia kazi kwa nafasi.
Tunaishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kujiandaa kutujengea jengo la Mahkama mpya kwa lengo la kutuimarishia miundo mizuri ya utendaji wa kazi kwa kila sekta .
“Tunashukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuweza  kutaka kutujengea   jengo hili kwani  jengo hili  sasa lishakuwa dogo halikidhi haja kwa wafanyakazi hivyo likimalizika huko tutaweza kufanya kazi zetu katika mazingira mazuri”, alisema Jaji huyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.