Kiongozi wa Msafara wa Umoja wa Wakala wa Ajira Binafsi Zanzibar Aman Khamis Fakih akizungumza na waandishi wa habari huko katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar wakati wakiondoka Kuelekea Nchini Oman..
Picha na Khadija Khamis Maelezo Zanzibar
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
Umoja wa Wakala wa Ajira Binafsi Zanzibar(ZAPEA) umeishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwapatia fursa ya kushiriki mkutano wa kimataifa nchini Oman kwa lengo la kukuza ajira nchini .
Hayo yameelezwa na Kiongozi wa Msafara Amani Khamis Fakih huko Uwanja wa Ndege wai Abeid Amani Karume wakati wakiondoka kuelekea nchini Omani .
Amesema wataitumia vyema fursa walioipata kwani wataweza kuondoa changamoto wanazokumbana nazo katika kazi zao kwa vijana wanapokuwa nchini huko.
Alieleza kuwa changamoto zinazojitokeza kwa baadhi ya vijana wanaokwenda kufanyakazi huko nchini Oman ni pamoja na kutofuata utaratibu wa ajira jambo ambalo husababisha migogoro na usumbufu wafanyakazi na waajiri wao.
Aidha alifahamisha kuwa Umoja wa Wakala wa Ajira Binafsi Zanzibar unapeleka wafanyakazi mbalimbali katika Serikali ya Oman kwa kuzingatia Sifa, Mkataba Sheria na vigezo ambavyo vinakubalika kisheria.
“Vijana wanaopelekwa na Umoja wetu katika nchi tofauti kwa masuala mazima ya ajira tunahakikisha tunazingatia vingezo muhimu vinavyohitajika na kutiliana saini Mkataba na Kampuni husika pamoja na kushirikiana na Serikali ya Zanzibar na Ubalozi”Alisema Amani
Nae Bi Khadija Said amewataka vijana kutokata tamaa katika kutafuta ajira nje ya nchi kwani serikali inafursa nyingi kupitia kwa wawekezaji.
Mkutano huo wa Kimataifa ni wa Siku tatu unafanyika nchini Oman ambao umetayarishwa kwa mashirikiano kati ya Serikali ya Oman na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .
No comments:
Post a Comment