Habari za Punde

Vijana Watakiwa Kutumia Teknolojia Katika Masomo Yao.

 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya amali Zanzibar Bakari Ali Silima akifungua Mafunzo ya uwasilishaji wa Teknolojia mpya ya internet thing huko Ukumbi wa Suza Vuga Mjini Zanzibar.
Mkufunzi wa Mafunzo ya Teknolojia mpya ya internet thing Sebastian kutoka chuo kikuu cha Teknolojia Coopenhagen Denmark akitoa mafunzo kwa Wanafunzi wa Vyui Vikuu vya Zanzibar huko Ukumbi wa Suza Vuga Mjini Zanzibar.
Na Mwashungi Tahir    Maelezo  17-10-2019.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Amali Zanzibar Bakari Ali Silima aliwataka vijana kuitumia teknolojia mpya ya internet thing kuitumia vizuri ili waweze kupata ukusanyaji ya mambo mbali mbali ya kijamii.
Akizungumza na vijana wa  huko kwenye Ukumbi wa Suza ulioko Vuga wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya Teknolojia hiyo ya internet thing na kuwataka vijana hao kuona  wanafaidika na mafunzo hayo.
Alisema Teknolojia hiyo itazidi kukuza vyuo vikuu kwa kuweza kusoma kwa urahisi na pia kufanya shughuli nyengine za kijamii ikiwemo kilimo na Uvuvi na kuweka matumaini ya maendeleo kwa vijana hao.
Aidha amesema teknolojia hiyo ina fursa nyingi kwa kutumia simu ya mkononi ambayo itaweza kukurahisishia katika kazi mbali mbali na kupata uwezo wa kujiajiri mwenyewe na kukuwezesha kufanya mambo mengi.
Mambo ambayo yanayoweza kukurahisishia kufanya ni pamoja na uvuvi kwa upande wa baharini na  nchi kavu unaweza kuitumia kwenye kilimo bila ya kwenda kwenye shamba na pia inaweza kuona kama CCTV kwa kuona wezi  wewe mwenyewe ukiwa kwenye nyumba yako.
Hivyo amewataka vijana kuitumia fursa hii ambayo inaweza kuwapatia ajira na kuweza kujiendeleza kimaisha na pia  kujiongeze utaalamu.
Nae Mkuu wa Skuli ya Elimu endelezi na utaalamu inahusiana na Teknolojia hii Dr Haji Ali Haji  amesema hii ni taaluma mpya kwa Zanzibar na kuwataka kuyazingatia mafunzo hayo wanayopatiwa na wakitoka hapo wakafanyie kazi.
Akitoa wito kwa vijana na kuwambia iwapo wataifanyia kazi teknolojia hii kutaweza kujiajiri wenyewe kukuza kipato na kuondosha umasikini katika kazi zao za kila siku pamoja na akinamama wajasiriamali wataweza kufaidika nayo.
Amesema teknolojia hii inarahisisha mambo mengi ikiwemo urahisishaji wa kuweza kutumia simu yako ya mkononi kwa kuingiza kila unachotaka ikiwemo kufanya utafiti wa kitu, mazingira na hata mambo ya utalii.
Kwa upande wa mtaalamu  wa mafunzo hayo kutoka chuo Kikuu cha Teknolojia cha Coopenhagen Dernmark Sebastian amesema teknolojia hii kwa vijana ni nzuri sana na kuwataka   waitumie vizuri kwani itawarahisishia mambo mengi kwa kutumia simu za mkononi.
Mafunzo haya ya siku moja yamewashirikisha vijana kutoka vyuo vikuu  mbali mbali vya Zanzibar na kuahidi watayafanyia kazi , ambapo kozi hii ya muda mfupi inatarajiwa kufunguliwa muda mfupi ujao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.