Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibaer Mhe.Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Maonesho ya Wajasiriamali ya Kuadhimisha Miaka 20 Kuazishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki s

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi Muombwa akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwenye Banda lao katika Maonyesho ya kusherehekea Miaka 20 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki huko Fumba.

Na.Othman Khamis.OMPR.                                                                                                                     
Mataifa Sita yanayounda Jumuiya ya Afrika Mashariki {EAC} yameanza kuchanja mbuga katika harakati zake za kuimarisha Uchumi ili kunufaisha Wananchi wake baada ya kipindi kirefu kilichoshuhudiwa sintofahamu ya vugu vugu za kisiasa kwa baadhi ya Mataifa hayo.
Wakati hayo yakishuhudiwa kutokana na kuongezeka kwa Pato la Taifa kwa Nchi Wanachama linalokadiriwa kufikia Dola za Kimarekani Bilioni 79, Jumuiya hiyo ya Afrika ya Mashariki inasherehekea kutimia Miaka 20 tokea kufufuliwa tena kwenye Makao Makuu yake Mjini Arusha Tanzania.
Maadhimisho hayo yaliyotanguliwa na Maonyesho ya Wajasiriamali na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein siku Tano zilizopita nayafanyika maeneo Huru ya Uwekezaji Fumba ambapo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipata fursa ya kuyatembelea.
Moja kati ya mambo aliyoyashuhudia Balozi Seif ni Ushiriki mkubwa wa Wajasiriamali kutoka Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wakionyesha kuchangamkia fursa mbali mbali za Uchumi ndani ya Jumuiya zinazoweza kustawisha maisha yao kutokana na mauzo ya bidhaa wanazozalisha.
Halkadhalika Taasisi na Mashirika ya Umma kutoka Serikali zote mbili Nchini Tanzania nazo hazikuwa nyuma katika kutangaza kazi na majukumu wanayowajibika nayo kila siku tukitolea mfano Kamisheni ya Utalii Zanzibar inayozidi kupaa katika harakati zake za kusimamia Sekta ya Utalii Nchini.
Afisa Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Nd. Amour Mkubwa Ali alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Taasisi hiyo kwa sasa  imejipanga vyema kuendelea kuutangaza Utalii katika Mataifa ya Kusini na Mashariki ya Afrika, Bara ya Asia pamoja na Mashariki ya Mbali.
Nd. Amour alisema juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Kamisheni hiyo ni pamoja na kuchapisha vipeperushi, vipindi vinavyoelezea Historia ya Utalii Zanzibar kwa kutumia Flash, CD pamoja na DVD na kuzisambaza kwa Mawakala wao wakitumia pia Afisi ya Kibalozi za Tanzania katika Mataifa tofauti Duniani.
Afisa Masoko huyo wa Kamisheni ya Utalii alieleza kwamba hatua hiyo imeisaidia sana Zanzibar kuendelea kufahamika na Mataifa mbali mbali Ulimwenguni jambo ambalo limepelekea kuongezeka kasi ya Uingiaji wa Watalii Visiwani Zanzibar katika kipindi kifupi kilichopita.
Alisema kwa Mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015 – 2020 Zanzibar kupitia usimamizi wa Kamisheni ya Utalii ililenga kupokea Watalii Laki 500,000 hadi ifikapo Mwaka 2020 wakati hivi sasa jumla ya Watalii Laki 520, 208 tayari wameshaingia Nchini hadi Mwaka 2018.
Nd. Amour alifahamisha kwamba matarajio mapya yaliyofanywa kipindi hichi baada ya uwepo wa mpango wa safari za uingiaji wa Watalii kutoka Nchini Urusi na Afghanistan yanatazamiwa kufikia Laki 700,000 ifikapo hapo Mwakani.
Jumuiya ya Afrika Mashariki au Mtangamano wa Afrika Mashariki (kwa Kiingereza East African Community, kwa  kifupi {EAC} ni muundo wa kisiasa unaounganisha Mataifa sita ya kanda ya Maziwa Makuu ya Afrika Mashariki
Mataifa hayo ni pamoja na Burundi, Jamuhuri ya KenyaRwandaSudan ya Kusini, Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Uganda yakiwa na Eneo la Mtangamano linalokadiriwa kuwa na urefu wa Kilomita Milioni 1,820,664.
Jumuiya yenye jina kama hilo imewahi kupatikana mara mbili katika  historia  iliyojumuisha Mataifa Matatu ya Jamhuri ya Kenya Uganda na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo mwaka 1967, lakini ilisambaratika mnamo Mwaka waka 1977.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.