Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya
watu Ofisi ya Taifa ya Kwimu (NBS), Bibi. Ruth Minja akifafanua jambo alikukuwa
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi
Oktoba 2019 leo jijini Dodoma. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na
Usambazaji Habari Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Bw. Said Ameir. asilimia 3.6
kutoka 3.4 kwa mwaka ulioshia Septemba 2019.
Na: Mwandishi Wetu,
MAELEZO -Dodoma
Mfumuko wa bei wa
Taifa kwa kipimo cha mwaka unaoishia mwezi Oktoba 2019 umeongezeka hadi
asilimia 3.6 kutoka asilimia 3.4 mwaka ulioishia mwezi Septemba 2019 ikiwa ni
ongezeko la asilimia 0.2.
Akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari kutangaza takwimu za bei, Kaimu Mkurugenzi wa
Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu, Bibi. Ruth Minja amesema kuwa ongezeko hilo
limetokana na kasi ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba,
2019 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi
Septemba2019.
Fahirisi za Bei
zimeongezeka hadi 115.84 mwezi Oktoba, 2019 kutoka 111.83 mwezi Oktoba, 209
“Ongezeko hili la
mfumuko wa bei limetokana na ongezeko la bei za bidhaa za Vyakula na Vinywaji
Baridi ambapo mfumuko wa bei kwa mwezi
Oktoba, 2019 umeongezeka hadi asilimia 5.1 toka asilimia 4.0 mwezi Septemba,
2019.” Alisema Bibi. Ruth.
Aidha amesema kuwa
mfumuko wa bei kwa bidhaa na huduma zote ambazo hazijumuishi chakula na nishati
kwa mwezi Oktoba, 2019 umepungua kidogo hadi asilimia 2.6 kutoka asilimia 2.6
kutoka asilimia 2.7 Septemba, 2019
Fahirisi za Bei kati ya mwezi Septemba, 2019 na
mwezi Oktoba, 2019 zimepungua kwa asilimia 0.1 ambapo badiliko ni sawa na
badiliko lilivyokuwa kati ya mwezi Agosti, 2019 na mwezi Septemba 2019
Alizitaja baadhi ya bidhaa zilizochangia kupungua
kwa fahirishi kuwa ni pamoja na mafuta ya taa kwa asilimia 2.5, dieseli kwa
asilimia 2.1, petrol kwa asilimia 4.0. vifaa kwa ajili ya uchakataji wa taarifa
kama kompyuta kwa asilimia 5.1 na baadhi ya huduma binafsi.
Tanzania kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)
ambayo ndiyo mamlaka ya kutangaza takwimu pamoja na nchi wanachama wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki imekuwa na utaratibu wa kutangaza matokeo ya mfumuko wa
bei kila mwezi ambapo ambapo mfumuko wa
bei katika nchi hizo utangazwa.
No comments:
Post a Comment