Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein Azungumza na Uongozi na Wafanyakazi wa Shirika la Magazeti ya Serikali ya Zanzibar leo.

  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwapongeza Wafanyakazi wa Shiriuka la Magazeti ya Serikali ya Zanzibar leo, akionesha Gazeti Jipya la (Zanzibar Mail Newspaper ) wakati wa mkutano wake na Wafanyakazi na Uongozi wa Shirika la Magazeti ya Serikali ya Zanzibar leo, uliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo.kushoto Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.Bi. Khadija Bakari na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magfharibi Unguja.Mhe.Hassan Khatib Hassan. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein alikutana na Uongozi na wafanyakazi wa Shirika la Magazeti ya Serikali.
Akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja zilizoibuliwa na wafanyakazi wa Shirika hilo, Dk. Shein alitaka kuwepo mashirikiano ya pamoja baina ya Menejment ya Shirika, Bodi, Wizara na Serikali Kuu ili kufikia mafanikio na kutaka  kila mmoja ana dhima ya kutekeleza wajibu wake.
Alisema lengo na  mipango ya Serikali  ni kuwa na Shirika lenye nguvu na linalojitegema wenyewe, litakaloweza kulipa mishahara, maposho, mahitaji ay usafiri an kutoa huduma nyingine mbalimbali.
Alisema mahitaji ya wafanyakazi na  mengineyo yatapaswa kuidhinishwa na Bodi ya Shirika hilo, sambamba na kuwashajiisha wafanyakazi kupenda kusoma, kwa kigezo kuwa Shirika linahitaji watu wenye taaluma ya kutosha.
Aidha, aliwapongeza wafanyakazi wa Shirika hilo kwa kazi nzuri ya kuendeleza gazeti hilo.
Alisisitiza umuhimu wa wafanyakazi kujikita katika kutafuta taaluma, kwa kigezo kuwa ndio msingi wa maendeleo yoyote Duniani.
Nae, Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulahamid Yahya Mzeee, aliutaka uongozi wa Shirika hilo kufanya mambo yake kwa uwazi, hususan katika suala la maslahi ya wafanyakazi (posho) na kufuata taratibu ili kuondoa manung’uniko miongoni mwa wafanyakazi.
Kuhusiana na suala la masomo, Dk. Mzee alisisitiza haja ya kuwepo programu maalum ya mafunzo kwa wafanyakazi, ili taasisi iweze kukidhi mahitaji yake ipasavyo.
Alisema kwa yale masomo yalio katika kada maalum, ambapo  mafunzo yake hupatikana nje ya nchi, ameelekeza mapendekezo ya namna hiyo yatumwe Serikali ili yaweze kuchukuliwa hatua.
Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Mahamoud Thabit Kombo alisema uwepo wa makundi na matabaka miongoni mwa watendaji wa shirika hilo ni jambo linalodumaza maendeleo ya shirika.
Alisema uongozi wa Wizara hiyo umejipanga kulishughulikia suala hilo ili ufumbuzi wa kudumu uweze kupatikana na kurudisha mshikamano kazini.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya serikali Yussuf Khamis alitowa pongezi kwa serikali kwa kulipatia makazi bora Shirika hilo, hivyo  kuwa katika mazingira bora zaidi ya kiutendaji.
Alisema wakati Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akitimiza miaka tisa ya uongozi wake, Shirika hilo linajivunia kuanzisha gazeti jipya  la ‘Zanzibar Mail’ linalochapishwa kwa lugha ya Kiingereza.
Katika mikutano hiyo wafanyakazi wa mashirika hayo mawili walipata fursa ya kuibuwa hoja katika nyanja mbali mbali, ikiwemo upatikanaji wa fursa za masomo, matatizo ya usafiri, ajira, usalama, posho la usumbufu na nyenginezo.

Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822 
E-mail: abdya062@gmail.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.