Habari za Punde

Uteuzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI)


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


TAARIFA KWA UMMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, alimteua Dkt. Felician Kilahama kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania, (TAFORI), kuanzia tarehe 8 Novemba, 2019.

Kufuatia hatua hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla (Mb), amewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania:-

(i)              Dkt. Khamisi Jumanne Kalegele
(ii)            Bw. Albert Gasper Msando
(iii)           Dkt. Ezekiel Edward Mwakalukwa
(iv)          Prof. Dos Santos Aristariki Silayo
(v)            Dkt. Nicepher Pius Lesio
(vi)          Dkt. Tuli Salum Msuya
(vii)         Bi. Neema Kichiki Lugangira
(viii)       Dkt. Deogratias Soka Matanda
(ix)          Dkt. Revocatus Petro Mushumbusi

Dkt. Mushumbusi anateuliwa kutokana na wadhifa wake kama Mtendaji wa TAFORI; atakuwa ndiye Katibu wa Bodi.

Uteuzi huu ni wa muhula wa miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 8 Novemba, 2019.
  
Prof. Adolf F. Mkenda
KATIBU MKUU
22 Novemba, 2019

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.