Habari za Punde

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Hemed Suleiman Azitaka Kamati za Utalii Pemba Kuanda Mipango Kazi

Na Miza Othman –Maelezo Pemba.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Hemed Suleiman Abdalla amezitaka kamati za utalii kuandaa mpango kazi utakao waongoza katika kamati hiyo ili waweze kutekeleza vizuri majukumu yao.
Aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya siku moja kwa kamati za Utalii za Wilaya ,Mkoa wa Kusini Pemba juu ya dhana ya Utalii kwa wote katika Afisi ya Maktaba Chakechake kisiwani Pemba.
Alisema kwa hivi sasa suala la Utalii ndilo lenye maslahi makubwa katika Nchi hivyo wanawajibu wa kuendeleza na kuuthamini ili kujiamini katika utendaji wa kazi zao katika sekta hiyo.
Hata hivyo alisema bado Mkoa wa Kusini unafursa kubwa ya Utalii na kufuata muongozo kwani kila mmoja anawajibu wa kusimamia, kujituma, kutoa michango nakufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo katika Nchi.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Chake chake Rashid Hadidi Rashid aliwataka wajumbe wa Kamati kuibuwa vituo mbali mbali vya utalii katika kisiwa chao na kutoa taaluma za kutosha kwa Wananchi wote.
Pia aliwataka kutumia mbinu mbalimbali za kuboresha miundombinu ya vivutio vya utalii ili kuondoa usumbufu wakati wageni wapakapo vitembelea  vituo hivyo na kuweza kufika kwa wakati.
Kwa upandewake  Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya kale Pemba Khatibu Juma Mjaja alisema Sekta  ya utalii ndio sekta mama hapa Zanzibar kwani ndio inayoongoza kukuza pato la ndani  katika Nchi hivyo wananchi kuwa tayari kuchangamkia fursa mbalimbali zitokazo na  Utalii ili kutatua huduma zinazowakabili.
Nao wajumbe wa Kamati hiyo waliwashukuru wakufunzi kwa kupatiwa elimu  ya utalii na wameahidi  watayafanyia kazi kama walivyoagizwa na ili wananchi hao waweze kufaidika kupitia sekta hiyo.
Jumla ya mada mbili ziliasilishwa ikiwemo Fursa na changamoto za maendeleo ya utalii Mkoa wa Kusini Pemba na Kamati za Wilaya na  utekelezaji wa dhana yauatlii kwa wote Kisiwani Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.