Habari za Punde

WAZIRI UMMY AMTEMBELEA MTOTO ANNA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akiwa na Mtoto Anna Zambi alipomtembelea nyumbani kwa mama yake Mdogo Mkoani Arusha
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu akiwa na Mtoto Anna Zambi na mama mdogo yake Anna Bi. Isabella Lyimo alipomtembelea nyumbani kwa mama yake Mdogo Mkoani Arusha.

 Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
Na. Mwandishi Wetu Arusha
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu leo amtembelea mtoto Anna Zambi ambae alipoteza wazazi wake wote wawili na wadogo zake watatu katika ajali iliyotokea Korogwe  Tanga, mwezi Octoba 2019. 

Waziri Ummy amemishi Mtoto Anna Zambi kujipa moyo na kujikaza na kumuomba Mungu amsaidie kumpa faraja katika kipindi kigumu anachokipitia baada ya kupotea wazazi wote na ndugu zake.

“Mimi nikutie moyo mtoto wangu tuko pamoja na Serikali haitokuacha peke yako tutajitaidi kukupa faraja kuwezesha kupata msaada wa huduma za msaada wa kisaikolojia taratibu na kwa uweza wake Mungu utarudi katika hali yako ya kawaida” alisema Mhe. Ummy

Kwa upande mama yake mdogo  mtoto Anna  Bi. Isabella Lyimo wamemshukuru Mhe Ummy kwa kumtembelea Anna na kuendelea kuwapa faraja.

Wazazi wa Anna- Lingston Zambi na Winfrida Lyimo pamoja na ndugu zake watatu Lulu, Adrew na Grace walifariki Dunia Oktoba 26 mwaka huu wakiwa njiani kutoka jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Kilimanjaro, kwenye mahafali ya Kidato cha Nne ya Anna, ambapo gari waliokua wakisafiria lilisombwa na maji na mafuriko yaliyotokea wilayani Handeni mkoani Tanga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.