JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
TAARIFA KWA
UMMA
Dodoma-Disemba
20, 2019.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe ametoa pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Wallace Karia kwa
kuchaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Soka
Afrika Mashariki na Kati CECAFA.
Dkt. Mwakyembe amesema kuwa wizara itaendelea kushirikiana Bw.Karia ili
kuhakikisha mafanikio ya CECAFA yanafikiwa katika kipindi cha uongozi wake
pamoja na kuendeleza soka la hapa nchini.
Bw. Karia anachukua nafasi ya Mutasim Gaffar wa Sudan aliyemaliza muda wake na ataongoza
shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka minne kuanzia sasa, huku akiwa Mtanzania wa pili kushika wadhifa
huo baada ya Bw.Leodger Tenga.
Aidha, nafasi ya Makamu wa Kwanza wa
Rais imechukuliwa na Francis Amin wa Sudan Kusini na nafasi ya Makamu wa Pili Rais imechukuliwa na Jira Isayaa kutoka Ethiopia.

Anitha Jonas
Kaimu Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
No comments:
Post a Comment