Habari za Punde

RAIS DKT MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA DARAJA LA KIGONGO-BUSISI (Km 3.2) JIJINI MWANZA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisaidiwa na Spika wa Jamhuri ya Muungano Mhe Job Ndugai akifunua kitambaa kuashiria uwekaji rasmi wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Daraja la  Kigongo-Busisi  lenye urefu wa Kilomita 3.2 kwenye sherehe iliyofanyika eneo la Kigongo jijini Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali akikata utepe kuanzisha rasmi kwa Ujenzi  wa Daraja la Kigongo-Busisi  lenye urefu wa Kilomita 3.2 kwenye sherehe iliyofanyika Kigongo jijini Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiangalia picha kubwa ya mfano wa  Daraja la Busisi-Kigongo lenye urefu wa Kilomita 3.2 baada ya kuweka jiwe la msingi na kuzindua rasmi kuanza kwa ujenzi wake kwenye sherehe iliyofanyika Kigongo jijini Mwanza

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipiga ngoma kwa furaha wakati wa sherehe za uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Daraja la Busisi-Kigongo lenye urefu wa Kilomita 3.2 kwenye sherehe iliyofanyika Kigongo jijini Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na msichana Salma Yasini, Kiongozi wa wanafunzi wa Shule ya msingi ya Iseni B ambaye amemkabidhi shilingi milioni  tano ukiwa ni mchango wake kusaidia ujenzi wa vyoo na madarasa shuleni hapo wakitokea kwenye sherehe za uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Kigongo-Busisi  lenye urefu wa Kilomita 3.2 kwenye sherehe iliyofanyika Kigongo jijini Mwanza leo Desemba 7, 2019.
Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.