Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Jaji Mkuu
wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na Waziri wa
Katiba na Sheria Balozi Agustine Mahiga kuashiria ufunguzi wa Jengo la Mahakama
ya Wilaya ya Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Jaji Mkuu wa Tanzania
Profesa Ibrahim Juma mara baada ya kufungua jengo la Mahakama ya Wilaya ya
Chato lililopo Mlimani Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa
Chato (hawaonekani pichani) wakati akiwasili katika viwanja vya Mahakama ya
Wilaya ya Chato mkoani Geita. Kulia ni Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim
Juma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua eneo la Mapokezi katika
jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Chato lililopo eneo la Mlimani Chato
mkoani Geita mara baada ya kulifungua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa
Chato mara ya kufungua jengo la Mahakama la Wilaya ya Chato.
Moja ya Vyumba vya Mahakama
hiyo ya Wilaya ya Chato kama inavyoonekana pichani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe kuashiria uwekaji wa
Jiwe la Msingi mradi wa ujenzi wa Kituo cha Jeshi la Zimamoto la Wilaya ya Chato mkoani Geita.
Sehemu ya Jengo la Kituo cha
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji cha Wilaya ya Chato kilichowekewa Jiwe la Msingi leo
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
Picha na Ikulu.
No comments:
Post a Comment