Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiondia kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Jengo la Michezani Mall Jijini Zanzibar (kushoto kwa Rais) Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa, hafla hiyo imefanyika katika eneo hilo michezani, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.
Ali Mohamed Shein amesema kuwa kulikuwa
kuna kila sababu ya kufanyika Mapinduzi matukufu ya Januri 12, 1964 ili kuleta
usawa na umoja sambamba na kuwafanya Waafrika waishi maisha bora.
Rais Dk. Shein
aliyasema hayo leo katika hotuba yake aliyoitoa katika hafla ya uwekaji wa mawe
ya msingi ya Michenzani Mall na jengo la Sheikh Thabit Kombo, hafla
iliyofanyika katika viwanja vya Mapinduzi Square, Michezani Mjini Zanzibar ikiwa
ni shamrashamra za sherehe za miaka 56 ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964.
Alisema kuwa Mapinduzi
yameleta usawa, umoja, udugu na maelewano na kubwa zaidi ni kuondosha ubaguzi
wa aina zote na kuwafanya watu wawe wamoja sambamba na kutandika mipango mipya
ya maendeleo.
Rais Dk. Shein alisema
kuwa Zanzibar inayoonekana leo na ile ya miaka 60 iliyopita ni tofauti na hivi
sasa kuna Zanzibar mpya iliyozaliwa Januari 12, 1964.
Akieleza historia ya
Zanzibar, Rais Dk. Shein alisema kuwa wazee walipata madhila na hawakuwa na
maisha mazuri kama ilivyo hivi sasa na kuwataka Wazanzibari kutosahau historia
yao ikiwa ni pamoja na kujua walikotoka, walipo na wanakokwenda.
Rais Dk. Shein
alitumia fursa hiyo kueleza historia ya mji wa Zanzibar na mipaka yake kabla ya
Mapinduzi matukufu ya Januari 12, 1964 na jinsi Waafrika walivyokuwa wakiishi
katika nyumba zisizostahiki kuishi binaadamu.
Katika historia hiyo,
alisema kuwa lazima historia ielezwe kwa watoto, wajukuu, virembwe na
vinyinginya hasa ikizingatiwa kuwa kabla ya Mapinduzi Mwafrika alikuwa hana
haki ya kufanya jambo lolote la maendeleo hata kustarehe nchini mwake.
Alisema kuwa hatua hiyo
ndio iliyopekekea mapambano ya miaka saba katika kupigania uhuru wa Mwafrika
hapa Zanzibar na hatimae kufanywa kwa Mapinduzi matukufu ya Januari 12, 2964.
Alisema kuwa ni jambo
la simanzi kwa wale wanaokebehi Mapinduzi kwani Mapinduzi yamefanyika nchi
nyingi duniani ikiwemo Ufaransa, Marekani, Cuba, Misri, China na nyenginezo kwa
lengo la kuondoa dhulma.
Aidha, Rais Dk. Shein
alisema kuwa Mapinduzi yalikuwa ni lazima yafanyike hapa Zanzibar ili wananchi
waishi katika mazingira mazuri na kuondokana na dhulma zilizokuwepo wakati huo
kabla ya Mapinduzi ili kuleta usawa na umoja.
Rais Dk. Shein
alitumia fursa hiyo kuieleza Sheria ya mwanzo Sheria namba 6, ambayo
ilisisitiza umoja, amani, maridhiano sambamba na kuishi pamoja kwani hayo ndio
malengo ya Mapinduzi.
Mapinduzi yamejenga
umoja na maelewano kwa wananchi wa Zanzibar wakiwemo wa Unaguja na Pemba.
Alileza kuwa
Michenzani ni kitovu na historia ya Mapinduzi na mambo yote wakati huo yalikuwa
yakipatikana Michenzani hivyo, ni vyema historia hiyo ikaimarishwa.
Rais Dk. Shein alisema
kuwa yeye hajazoea kuwadanganya wananchi kwani aliahidi kuwa atajenga Michezani
Mall na ndivyo alivyofanya licha ya baadhi ya watu wachache kuibeza ahadi yake
hiyo.
Alisema kuwa jengo la
Thabit Kombo linatokana na historia ya muasisi huyo ambaye ameitumikia nchi na
anahistoria kubwa ya Zanzibar sambamba na historia ya biashara na historia ya
ASP na baadae CCM.
Alisema kuwa Awamu ya
Saba imeamua kuendeleza historia yake kwa kujenga mji mpya wa Kwahani ambapo
ujenzi umeanza tayari na Shirika la ZSSF limekuwa likiekeza kwa maelekezo ya
Serikali.
Alisema kuwa wafanyabiashara
waliohamishwa wawe ndio wa mwazo kwani wameipisha Serikali ikajenga hivyo ni
lazima watekelezewe ahadi waliyoahidiwa
ili kuepuka kuja kuwaudhi na kupelekea
kuinunia Serikali yao.
Rais Dk. Shein alieleza
mipamgo ya Serikali ya kujenga majengo zaidi sambamba na kujenga miji mengine
midogo ukiwemo Chumbuni, Chwaka, Mkokotoni, Tunguu na mengineyo.
Alisema kuwa Serikali
ina mpango wa kuanzisha Kampuni yake ya Ujenzi ili kuepusha gharama za ujenzi
na kujenga majengo makubwa sambamba na kuweza kushindana na Kampuni nyengine.
Aliipongeza ZSSF na
kueleza kuwa anaimani kwamba uongozi uliopo utafanya mambo mazuri zaidi ambapo
pia, alitumia fursa hiyo kuipongeza Maskani Kaka ya MwembeKisonge kwa kukubali kiwanja
chao kiwekezwe na ZSSF kwa lengo la kupata mafanikio.
Ameeleza kufurahishwa
na mashirikiano mazuri yaliopo kati ya Maskani ya CCM ya Mwembekisonge na Shirika
la ZSSF na kuwataka Wanamaskani wa maskani hiyo kuekeza vizuri na kuzitumia rasilimali
hizo ili kuweza kupata tija.
Alisisitiza kuwa
Zanzibar itaendelea kunawiri kwani Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar si Serikali
ya wababaishaji kwani inatekeleza yale yote iliyowaahidi wananchi.
Alieleza kuwa ni jukumu
la wananchi wote kuyalinda na kuyadumisha Mapinduzi matukufu ya Januari 12,
1964 kwani Mapinduzi ni mabadiliko ambayo yameondosha yake yote yaleyaliokuwa
hayako sawa.
Alisemakuwa jukumu la
wananchi mnikuyalinda na kuyaendeleza Mapinduzi kwani bado safari ya kuendelea
kufanya vizuriinahitajika hsa kukiwa na lengo lakuwa kila Wizaya na Mkoa kuwa
na Mall zake.
Rais Dk. Shein
aliwaeleza wananchi kuwa ni matarajio iwapo mradi wa mafuta na gesi utakwenda
vizuri Zanzibar itazidi kupata mafanikio zaidi ambapo mambo mengi
yatafanikishwa.
Mapema Rais Dk. Shein
aliweka mawe ya msingi katika jengo la Michenzani Mall na jengo la Sheikh
Thabit Kombo liloopo Mwembekisonge na kuweza kupata maelezo juu ya ujenzi wa
majengo hayo kutoka kwa Abdulazizi Ibrahim Idd Meneja Mipango, Uwekezaji na
Utafiti wa ZSSF.
Nae Waziri wa Fedha na
Mipango Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa alisema kuwa eneo hilo lina historia
yake katika vuguvugu la Mapinduzi ya Januari 12, 1964.
Aliongeza kuwa miradi
hiyo miwili iliyowekewa mawe ya Msingi hivi le ni mimgoni mwa utekelezaji wa
Ilani ya Uchaguzi ya CCM sambamba na utekelezaji wa Dira ya 2020 ambapo matumaini yake kuwa kazi
ya kukamilisha majengo hayo itakwenda vizuri na matarajio ni kuzinduliwa na Rais
Dk. Shein.
Alisema kuwa ujenzi wa
jengo la Sheikh Thabit Kombo limeonesha mashirikiano mazuri na jina la Sheikh
Thabit Kombo limesibu huku akitumia fursa hiyo kusisitiza haja ya kuwaezi wazee
na waasisi wa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Aliwataka wananchi
wasiwe na wasiwasi juu ya miradi ya uwekezaji ya ZSSF kwani miradi yote
inafanyiwa upembuzi wa kutosha kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwawekeza
mazingira mazuri wananchi wake.
Nae Naibu Katibu Mkuu
wa CCM Zanzibar Abdalla Juma Sadalla Mabodi alitumia fursa hiyo kutoa salamu za
pongezi kwa Rais Dk. Shein kwa uongozi wake mahiri na wenye mfano akiwa ni Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia, ni Makamo wa CCM
Zanzibar.
Alisema kuwa umahiri
wake wa kuiongoza Serikali unaonekana mpaka katika kukiongoza Chama hatua ambayo
imepelekea maendeleo makubwa na uongozi uliotukuka sambamba na mashirikiano
anayoyaonesha kati ya Serikali na CCM.
Alisema kuwa umuhimu
wa maskani ya Mwembekisonge na Kachorora kwani ni maskani hizo zinahistoria
yake hapa nchini.
Naibu Katibu Mkuu huyo
alipongeza hatua zilizochukuliwa katika ushirikiano wa Chama na Serikali katika
kuhakikisha maendeleo ya wananchi yanapatikana na kueleza kuwa wameanza
kuonesha mfano kwani maskani hiyo imejengwa na ZSSF.
Alisema kuwa hivi sasa
kuna mazungumzo juu ya uendeshaji wa eneo la chini na ghorofa ya kwanza kwa
ajili ya CCM kwa lengo la kupata kipato hasa ikizingatiwa kuwa chama hicho kina
mwelekeo katika ushindi wa chama hicho sambamba na kujiimarisha kiuchumi ili chama kiweze kujiendesha wenyewe.
Nae Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mipango Khamis Mussa katika risala yake alisema kuwa ujenzi
wa maduka hayo katika eneo la Michenzani ni miongoni mwa utekelezaji wa Ilani
ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020 ambayo kwa
Zanzibar, Rais Dk. Shein amekuwa akiitekeleza kwa vitendo.
Alieleza kuwa usanifu
wa jengo la Michenzani Mall umefanywa na Kampuni ya ARQES AFRICA kutoka Dar –es
Salaam na ujenzi wake unafanywa na Kampuni ya CRJE- East Africa pia ya Dar-es
Salaam yenye asili ya China ambapo mkataba wa ujenzi huo ulisaniwa Oktoba 4,
2018 kwa gharama ya Bilioni 27.9 ikiwa ni pamoja na VAT.
Alieleza kuwa ujenzi
wa maduka hayo utakuwa na urefu wa mita 35 na ghorofa 9 ambapo ghorofa ya hini
ya ardhi atatumika kama ni ghala kwa ajili ya kuhifadhi bidhaa za
wafanyabiashara wa jengo hilo na ghorofa ya chini itakayotumika kwa ajili ya
huduma za benki na sehemu za maduka ya kufanya biashara.
Aidha, alisema kuanzia
ghorofa ya tatu litagawika katika sehemu tau ambazo zinaanzia ghorofa ya tatu
hadi saba ambapokutokana na mahitaji ya afisi yanayojitokeza kilasiku, sehemu
mbili za duka hilo itakuwanisehemu za afisi.
Aliongeza kuwa sehemu
ya katikati ambayo ina jumla ya ghorofa saba itakuwa na ukumbi wa mikutano,
sherehe za harusi na sherehe nyenginezo wenye uwezo wwa kubeba hadi watu 500,
sinema ya kisasa pamoja na sehemu ya kufanyia mazoezi (GYM).
Katibu Mkuu huyo
alisema kuwa ujenzi huo umezingatia walemavu kwa kuwekwa “ramp” katika sehemu
za kuingia katika jengo,vyoo maalum kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum pamoja
na lift saba ambazo zinaweza kuwafikisha katika maeneo tofauti ya jengo.
Alisema kuwa kupitia jengo
hilo la Michenzani Mall kwa upande wa ZSSF itakuwa wameitekeleza dhana ya Rais
Dk. Shein kwa vitendo kwani kiasi cha sehemu 100 za biashara tofauti zitakuwepo
kwani aliwahi kusema kwamba
“Sasa basi tena
kufanya biashara mitaani, nataka biashara zishamiri katika maeneo maalum ya
biashara, na hivi ndivyo katika nchi za wenzetu wanavyofanya”.
Alisema kuwa
Mkandarasi aliahidi na kukubali kujenga kwa muda wa miezi 21 baada ya
kukabidhiwa eneo na tayari ameshatumia muda wa miezi 15 tokea kuanza ujenzi.
Alisisitiza kuwa ASSF
kwa kushirikiana na mshauri wa ujenzi watasimamia muda huo na kwa ujenzi wa
kiwango kinachotakiwa ambapo Kampuni ya CRJE inajenga mradi huo kwa thamani ya
TZS Bilioni 27.900 pamoja na VAT.
Kwa upande wa jengo la
Sheikh Thabit Kombo alisema kuwa huo ni ubia kati ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
Zanzibar (ZSSF) na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika eneo la maskani ya
MwembeKisonge kwa ajili ya mradi wa jengo la biashara lenye maduka, ofisi na
kumbi za mikutano.
Alisema kuwa baada ya
tathmini kufanyika Kampuni ya Group Six International Ltd YA Dar –es-Salaam
ambayo ina asili ya China ilichaguliwa kwa kuwa ndio kampuni iliyowashinda
wenzake kivigezo lakini ilichaguliwa kwa kuwa ndio yenye gharama ndogo za
ujenzi kwa mradi huo kwa gharama ya TZS Bilioni 9.71.
alisema kuwa mradi huo
utahusisha ujenzi wa ghorofa tano ikiwemo ghorofa ya chini ya ardhi
itakayotumika kwa ajili ya maegesho ya gari, ghorofa ya chini na ya kwanza
zitakazokuwa na maduka 40 ya biashara.
Aliongeza kuwa ghorofa
ya pili na ya tatu ya jengo hilo la Sheikh Thabit Kombo zitakwua ni ofisi
zitakazokodishwa kwa wananchi.
Alisema kuwa ujenzi
huo hauhamishi maskani ya Mwembekisonge, maskani Kaka bali maskani itaendelea
na shughuli zake kama kawaida ndani ya jengo katika ghorofa ya chini ilizopo
mbele ya jengo upande wa barabarani.
Sambamba na hayo,
katibu Mkuu huyoa lisema kuwa ZSSF hivi sasa imo katika hatua za kujenga jengo
jengine la kuegesha gari kwa juu ambalo kwa Zanzibar litakuwa la kwanza ambalo
linatarajiwa kujengwa pembezoni ya Michezani Mall na linaplenga kuondosha
tatizo la maegesho ya gari kwa
watakaokuwa wakifika maeneo hayo.
Rajab
Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment