Habari za Punde

SMZ na Jamhuri ya Cuba wasaini mkataba wa uimarishaji huduma za afya Zanzibar

 Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed na Balozi wa Cuba Professor Lucas Domingo Hernandez  wamesaini Mkataba wa uimarishaji huduma za afya kwa wananchi wa  Zanzibar, Hafla hiyo imefanyika  huko Ofisini kwake Wizara ya Afya Mnazimmoja .
 Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed na Balozi wa Cuba Professor Lucas Domingo Hernandez wakikabidhiana hati za mkataba  ambapo  hafla hiyo ilifanyika   huko Ofisini kwake Wizara ya Afya Mnazimmoja 
 Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed na Balozi wa Cuba Professor Lucas Domingo Hernandez wakipeana mikono mara tu baada ya kusaini mkataba huko Ofisini kwake Wizara ya Afya Mnazimmoja 
 Balozi wa Cuba Professor Lucas Domingo Hernandez akiishukuru Serikali ya Zanzibar Kwa kuonyesha mashirikiano katika hafla ya utiaji wa saini huko ofisini kwake  Mnazimmoja 
 Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed akitoa maelezo mafupi kwa  Balozi wa Cuba Professor Lucas Domingo Hernandez  mara tu baada ya kutiliana saini mkataba katika hafla iliyofanyika huko ofisni kwake  Mnazimmoja ,
PICHA ZOTE NA KHADIJA KHAMIS MAELEZO ZANZIBAR 
 


Na Mwashungi Tahir    Maelezo   
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Cuba imetiliana saini  mkataba wa uimarishaji  wa huduma za Afya kwa lengo la kuwasaidia wananchi wanaosumbuliwa na maradhi mbali mbali hasa ya sukari ambayo yatapatiwa chanjo maalumu ya ukaushaji vidonda  
Hafla  hiyo ya utiaji saini umefanyika huko Ofisini kwake  wa Wizara ya Afya Mnazi mmoja baina ya Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed na Balozi wa Cuba Professor Lucas Domingo Hernandez mkataba ambao una lengo la kuimarisha afya kwa wananchi wa  Zanzibar.
Waziri Hamad amesema Cuba wana mashirikiano makubwa katika masuala ya kuboresha mambo mengi ya maendeleo ikiwemo Afya, elimu na Kilimo.
Amesema Nchi ya  Cuba inongoza katika mambo mbali mbali ya afya na pia madaktari wa Zanzibar wanapatiwa mafunzo ya kutoa huduma kwa wagonjwa yenye lengo la kuimarisha  ujuzi zaidi  wa kimatibabu nchini.
Aidha amesema mafanikio mengi yamepatikana kutoka nchini huko ikiwemo kuwaleta madaktari bingwa kuja kuwatibu wagonjwa na  kutoa elimu ya kitaalamu kwa madaktari wa Zanzibar ambapo nchi yao inaongoza kwa kutoa huduma ikiwemo matibabu.
Nae Balozi wa Cuba profesa Lucas Domingo  amesema hivi sasa wamevumbua dawa inayoitwa HEBER PROT –P ambayo inakausha vidonda vya sukari na kuwaondoshea wagonjwa wa maradhi hayo kukatwa miguu au viungo vyengine.
Amesema baada ya kuonekana wagonjwa wengi wa sukari wanapopata vidonda Zanzibar na  kushindikana kutibika hadi kupelekea kukatwa miguu au baadhi ya viungo vyengine hivyo dawa hiyo itasaidia kuondosha na badala yake inapelekea kukauka kwa vidonda hivyo .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.