Habari za Punde

Ufunguzi wa Mkutano wa Mpango wa Kuhimili Ushindani wa Biashara Zanzibar.

 
Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe.,Balozi Amina Salum Ali akifungua mkutano wa Wajasiriamali kuhusiana na mkakati wa ushindani wa Kibiashara Nchini uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar.
Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar  20/01/2020
Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali amesema ushindani wa bidhaa nchini  unahitaji  mpangilio  maalum unaotokana na sera, sheria pamoja na soko la uuzwaji wa bidhaa hizo .
 Hayo ameyasema wakati akifungua Mkutano wa Wajasiriamali kuhusiano na Mpango wa kuhimili ushindani wa kibiashara  nchini huko katika Hoteli ya Verde Maruhubi .
Alisema ushindani wa biashara unahitaji mpangilio kwa kutoa mafunzo ya uzalishaji wa bidhaa kwa wajasiriamali ili kuweza kufuata maadili  ya wataalamu kwa kukuza uzalishaji na kuongeza kipato kwa wafanyabiashara wadogo wadogo.
Alisema kuwa wajasiriamali wa bidhaa ya mwani wameweza kupatiwa mafunzo ya mwani wa aina mpya ambayo unauwezo wa kutoa mbegu ya mwani kwa wingi hadi mashamba  kuimarika na kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa hiyo .
Aidha alisema Wajasiriamali waliopata mafunzo kwa upande wa Pemba ni katika Kijiji cha Makangale ,Tumbe ,Chokocho pamoja na Kusini, Kaskazini na Magharibi kwa Upande wa Unguja .
Alifahamisha kuwa changamoto zilizopo kwa wasiriamali hao ni ukosefu wa baadhi ya vifaa vya kufanyia kazi pamoja na boti ya uokozi pia wanahitaji  mafunzo ya uokoaji na upigaji mbizi  .
Alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar tayari imeshatiliana Mkataba katika Kampuni mbili tofauti pamoja na Utayarishaji wa ujenzi wa kiwanda cha mwani.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa  Dr.Donald Mmari amesema wamekuwa wakishughulikia sera ya masoko ya ndani na ya nje ya bidhaa mbali mbali ikiwemo bidhaa za mbogamboga ngozi pamoja na zao la  mpunga kwa lengo la kuimarisha bidhaa hizo ili ziweze kuingia katika ushindani wa kIbiashara .
Alifahamisha kuwa kwa upande wa bidhaa ya mwani huwasaidia kipato kwa wakulima wa mwani kutokana na kukuwa kwa uzalishaji wa bidhaa hiyo na kuweza kumiliki soko la ushindani
Alisema sera ya viwanda ina lengo la kukuza uzalishaji wa bidhaa kwa kukidhi mahitaji ya masoko pamoja na kuweza kuingia katika soko la ushindani .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.