Habari za Punde

Uwekaji wa Jiwe la Msingi Ofisi ya Hifadhi Visiwa Vya Changu na Bawe Zanzibar.(CHABAMCA)

Na Mwashungi Tahir - Maelezo Zanzibar.
Waziri wa Katiba na Sheria.Mhe. Khamis Juma Mwalim alisema sekta ya uvuvi ni muhimu katika kutoa ajira na mapato kwa wavuvi na wadau wengine pamoja na kukuza uchumi wa nchi  kwa ujumla.
Hayo aliyasema huko Mazizini Wilaya ya Magharibi “B” ikiwa ni shamra shamra ya kusherehekea sherehe  za kutimiza miaka 56 ya Mapinduzi Matukufu wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi katika Afisi ya Hifadhi ya Changuu-Bawe (CHABAMCA,
Alisema uanzishwaji wa maeneo ya hifadhi ni muhimu kwani ndio njia pekee ya muafaka ya kuhakikisha kunakuwa na matumizi endelevu ya rasilimali ya baharuini.
Aidha alisema Visiwa vya Unguja na Pemba rasilimali za bahari ndio tegemeo kubwa kwa maisha ya jamii ya wavuvi kwani zinatoa mchango mkubwa kwa sekta mbali mbali za kiuchumi zikiwemo utalii na uvuvi.
Hivyo alisema maeneo ya hifadhi za bahari zina nyasi bahari na matumbawe ambayo ni muhimu kwa samaki kuzaliana na kukua hupelekea wananchi kupata ajira , mapato na lishe bora inayotokana na samaki wanaovuliwa katika maeneo hayo.
Pia  alisema maeneo hayo huwa vivutio kwa watalii  wanaopenda kuogelea na kufurahia mandhari nzuri ya chini ya bahari na kupelekea wananchi wanaopeleka watalii katika maeneo hayo kupata fedha kutokana na biashara ya utalii wa mazingira.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha hifadhi ya bahari visiwani humo kwa lengo la kuhakikisha usimamizi wa hifadhi unaimarika kwa maeneo  hayo na kuomba  ushirikiano wa pamoja kwa wadau wote wanaotumia sehemu hiyo.
Aidha alisema kuwepo kwa jengo hilo la Afisi ya kisasa karibu na eneo la hifadhi kutaleta faida ya kutarahisisha utaratibu wa shughuli za doria , utaratibu wa shughuli za utafiti , utoaji wa elimu ya mazingira kwa jamii na kuimarisha ulinzi wa eneo hilo.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo , Maliasili , Mifugo na Uvuvi Omar      Ali alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia wizara hiyo imeamua kujenga Afisi ya Hifadhi ya CHABAMCA katika eneo hilo kutokana na kutokana na harakati nyingi za masuala ya uvuvi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mjini  Magharibi Hassan Khatib Hassan alisema katika mkoa wake hatolifumbia macho suala la udhalilishaji kwa wanawake na watoto .
Na pia atahakikisha ataidumisha amani na utuluivu izidi kutawala ndani ya Mkoa wake na pia anawaomba vyuo vya amali vituo mafunzo ya uvuvi ili vijana waweze kupata ajira .
Jumla ya shilingi milioni mia tatu ishirini na tisa laki tisa ishirini na tatu elfu mia mbili khamsini na tano na senti mbili (329,923,255.2/=ambapo fedha hizo zimetolewa na mradi wa usimamizi wa Uvuvi wa kanda ya Kusini Magharibi ya bahari ya Hindi (SWIOFish).
Mradi huo unatekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Benki ya Dunia World.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.