Habari za Punde

Wajumbe wa kamati ya Fedha Biashara na Kilimo ya BLW Zanzibar wakutana na wakulima na zao la karafuu Pemba

 MWENYEKITI wa kamati ya Fedha biashara na kilimo ya baraza la Wawakilishi Zanzibar, Dr. Mwinyihaji Makame Mwadini  akizungumza katika kikao cha pamoja baina ya wajumbe wa kamati hiyo, wakulima wa zao la Karafuu na wafanya biashara wa Karafuu na watendaji wa wizara ya biashara na shirika la ZSTC Pemba,  juu ya hali halisi ya zao hilo linavyoendelea.(PICHA NA ABDI SULEIMAN)
 MAAFISA wadhamini Kutoka shirika la biashara la Taifa ZSTC Pemba Abdalla Ali Ussi kulia na afisa Mdhamini Wizara ya biashara na Viwanda Pemba Ali Suleiman Abeid katikati, wakifuatilia kwa makini kikao cha wajumbe wa kamati ya Fedha biashara na Kilimo ya baraza la Wawakilishi Zanzibar na wakulima wa zao la Karafuu Pemba, kikao kilichofanyika Wete .(PICHA NA ABDI SULEIMAN)
 BAADHI ya wajumbe wa kamati ya Fedha biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa kamati hiyo Dr Mwinyihaji Makame Mwadini wakati alipokuwa akizungumza na wakulima na wafanyabiashara wa zao la karafuu Pemba .(PICHA NA ABDI SULEIMAN)
 NAIBU katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar Khadija Khamis Rajab, akizungumza wakati wa kikao cha pamoja baina ya wajumbe wa kamati ya Fedha Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakulima wa Zao la Karafuu na wafanyabiashara huko Wete .(PICHA NA ABDI SULEIMAN)
MKULIMA wa zao la Karafuu Mkoa wa Kaskazini Pemba Issa Juma, akitoa ufafanuzi juu ya mambo mbali mbali wanayokumbana nayo katika msimu huu wa zao hilo, kwa wajumbe wa kamati ya Fedha Biashara na Kilimo ya baraza la Wawakilishi Zanzibar ilipokutana na wakulima hao huko Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.