Habari za Punde

Chama Cha Mapinduzi Chatoa Siku 30 Kukamilika Kwa Mradi wa Maji Katika Kijiji cha Kilindini Wilaya ya Micheweni Pemba.

 
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Ndg Hamphrey Polepole akiwa katika ziara yake Kisiwani Pembe kutembelea Miradi mbalimbali ya Maendeleo ya Maji katika Wilaya ya Micheweni Kijiji cha Kilindini kuangalia mradi wa usambazaji wa maji safi na salama kwa Wananchi .

Akiwa katika ziara ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, Wilaya ya Micheweni, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Ndugu Humphrey Polepole amesema Chama Cha Mapinduzi kimetoa siku 30 kukamilishwa kwa mradi wa maji Wilaya Micheweni Pemba.
Hatua hiyo imekuja baada ya Ndugu Polepole kufika katika eneo la Kilindini ambapo kuna chanzo cha maji kinachopasa kupeleka maji kwa kilometa 4.6 hadi eneo la Micheweni lakini mradi huo umekuwa ukisua sua kwa muda mrefu na kuelekeza kukamilika kwa haraka kwa mradi huo wa maji ili kurahisisha huduma za kijamii na Kiuchumi katika Wilaya ya Micheweni.
Katibu wa Itikani na Uenezi CCM Ndh Hamphrey Polepole akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kilindini Wilaya ya Micheweni Pemba wakati wa ziara yake katika Mikoa miwili ya Pemba kuangalia Miradi ya Maendeleo. utekelezaji wa Ileni ya CCM kwa Wananchi.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.