Habari za Punde

SerikaliKupandaMitiBilioni 1 Mlima Kilimanjaro



Na. Immaculate Makilika – MAELEZO                                                                                    
Serikali imeandaa programu mbalimbali za kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na kupanda miti zaidi ya bilioni moja katika eneo la Mlima Kilimanjaro ili kukabiliana na matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi.

Akijibu swali Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.Mhe. Mussa Zungu alisema,“Programu ya kwanza ni kupanda miti zaidi ya bilioni moja katika eneo la Mlima Kilimanjaro ili kulinda barafu iliyopo katika nchi yetu, pamoja na kuanza mkakati wa kuomba fedha zilizopo katika Mfuko mpya ulioanzishwa na nchi ya Ufaransa, wa dola za kimarekani bilioni 100, ulioanzishwa kwa lengo la kuboresha mazingira katika nchi zenye uhitaji, ikiwemo Tanzania”.

Aidha, Waziri Zungu aliongeza kuwa mkakati huo wa kupanda miti na kuitunza hivi sasa unaandaliwa katika wilaya zote nchini, na miti itakayopandwa katika kila wilaya itakuwa ya aina maalumu ili kuendana na mazingira yaliyopo katika wilaya husika.

“Nchi yetu imebarikiwa kuwa na asilimia 39.9 ya misitu, misitu hii inapotea, kuanzia mwaka  1990 hadi mwaka 2010 tumeshapoteza takribani ekari milioni 8 ya misitu, na hii ni hatari kubwa sana kwa watanzania,  tuhakikishe tunaacha kukata miti,  tutumie miti kama fursa ya kibiashara, badala ya kuikata tuweke mazao ya nyuki”, amesisitiza Waziri Zungu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.