Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Watu wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta Ajumuika na Wananchi wa Kenya Katika Kutoa Heshima za Mwisho kwa Mwili wa Rais Mstaafu Daniel Toroitich Arap Moi.

Mwili wa rais mstaafu wa Kenya Daniel Toroitich Arap Moi umewasili katika bunge kutoka chumba cha kuhifadhi maiti cha Lee Funeral jijini Nairobi mapema leo.
Wakenya kutoka matabaka mbalimbali tayari wameanza kuutazama mwili huo wa kiongozi huyo wa zamani .
Hatua hiyo inajiri baada ya rais Uhuru Kenyatta aliewasili kutoka nchini Marekani mapema leo kuwa mtu wa kwanza kuutazama mwili huo.
Uhuru alipokewa na naibu wake wa rais William Ruto na mkuu wa majeshi Samson Mwathethe huku usalama ukiimarishwa.
Ruto aliwasili katika majengo ya bunge mwendo wa saa tatu na dakika 50 akiandamana na maafisa wa serikali.
Kwa sasa viongozi mbalimbali wanautazama mwili huo.
Msafara wa gari lililokuwa likiusafirisha miwli huo kutoka chumba cha Lee ulipitia barabara ya alley Road na kuingia Kenyatta Avenue kabla ya kuingia katika barabara ya bunge ambapo gwaride la kijeshi lilifanywa kutoa heshima.
Moi ambaye aliaga dunia siku ya Jumanne akiwa na umri wa miaka 95 atazikwa nyumbani kwake huko kabarak katika kaunti ya Nakuru tarehe 12 mwezi Februari.
Serikali ilitangaza siku ya Jumanne tarehe 11 mwezi Februari kuwa siku kuu kwa raia kushiriki katika ibada ya mazishi ya mwili wa kiongozi huyo wa zamani.
Kwa sasa wananchi waliopanga milolongo mirefu wamepewa fursa kuutaza mwili huo .Shuguli ya kuutazama mwili huo itafanyika kwa siku tatu hadi lkufikia Jumatatu.
Wakati rais Uhuru Kenyatta alipowasili katika majengo ya bunge kutoa heshima zake za mwisho kwa marehemu rais Mstaafu Daniel Moi

Rais Uhuru Kenyatta na mkuu wa majeshi Meja jenarali samuel Mwathethe
 Rais Uhuru Kenyatta na mkewe wakitoa heshima zao za mwisho kwa rais mstaafu Danile Moi
Wakenya waliojitokeza katika maeneo ya bunge la Kenya ili kutoa heshima zao za mwisho kwa rais mstaafu Daniel arap Moi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.