Habari za Punde

Wananchi wa Wilaya Magharibi B Unguja Watakiwa Kujitokeza Kuhakiki Taarifa Zao Katika Daftari la Wapiga Kura -RAWWAZA

Na.Takdir Suweid Maelezo Zanzibar,
Wananchi wametakiwa kujitokeza kujihakiki majina yao katika Daftari wa kudumu la wapiga kura ili kupata sifa ya kupiga kura.
Wito huo umetolewa na Katibu wa Jumuiya Rafiki ya Wanawake na Watoto (RAWWAZA) Tatu Hassan Abdallah amesema ili Mwananchi aweze kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu hakuna budi kuenda kujihakiki katika Daftari hiyo.
Akifanya ziara ya kukaguwa Vituo vya Uandikishaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura katika Wilaya ya Magharibi B Katibu wa Jumuiya Rafiki ya Wanawake na Watoto Zanzibar  RAWWAZA Tatu Hussein A bdallah amewaomba Wanaharakati na Taasisi mbalimbali kuunga mkono Serikali kwa kuhamasishana Wananchi kushiriki katika Daftari linaloendelea amewahimiza.
Aidha amesema kitendo cha kutokwenda kuhakiki majina yao kwa madai ya kuwa wanavyovitambulisho vya zamani ni kujikosesha haki zao za msingi ya kupiga kura.
Mbali na hayo wameipongeza Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC kwa kuipa kibali cha Uaangalizi katika Daftari la kudumu la Wapiga kura linaloendelea katika Wilaya ya Magharibi B.
Kwa upande wake Balozi wa Jumuiya ya Rawwaza Maryam Ali Maalim amesema kupiga kura ni haki ya kila Mtu hivyo ni vyema kufuata Utaratibu na Sheria zilizowekwa na Serikali ili waweze kupata haki zao za Msingi.
Nao baadhi ya wasimamizi wa vituo vya Uchaguzi katika Wilaya hiyo wamesema zoezi hilo limeendelea vizuri na kuwaomba Wananchi kuendelea kudumisha Amani na Utulivu iliopo nchini ili izidi kuimarika.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.