Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Afungua Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Katika Sekta ya Madini Tanzania wa 2020.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa  akikata utepe kuzindua  Utoaji wa Cheti cha Uhalisia kwa Madini ya Bati kwenye  ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha cheti baada ya kuzindua  utoaji wa  cheti cha uhalisia   kwa Madini ya Bati kwenye ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Februari 23, 2020. Kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai, wa pili kushoto ni Waziri wa Madini Doto Biteko na kushoto ni  Waziri wa Nchi Anayeshughulikia Maendeleo ya Madini wa Uganda,  Sarah Opendi
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vito vilivyotokana na madini ya Tanzanite wakati alipotembelea banda la kampuni ya GEM TANZANITE LIMITED katika maonesho yaliyokwenda sambamba na Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Katika Sekta ya Madini Tanzania wa Mwaka 2020  ulioufungwa na Waziri Mkuu kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Februari 23, 2020.  Wa pili kushoto ni Waziri wa Madini, Doto Biteko na watatu kulia ni Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama madini wakati alipotembelea banda la kampuni ya Kisangani Smith Group ya mkoani Njombe katika maonesho yaliyokwenda sambamba na Mkutano wa Kimataifa  wa Uwekezaji Katika Sekta ya Madini Tanzania wa Mwaka 2020 ulioufungwa na Waziri Mkuu kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar  es salaam, Februari 23, 2020.  Kushoto ni Waziri wa Madini, Doto Biteko na watatu kushoto ni Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofunga Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Katika Sekta ya Madini Tanzania wa mwaka 2020 kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha  Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Februari 23, 2020.
 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.