Dk. Shein alikutana na uongozi wa Wizara ya
Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo chini ya
Waziri wake Balozi Ali Abeid Karume ambapo Waziri huyo alieleza
kuwa Wizara hiyo imefanikiwa kutekeleza
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 kwa kiasi kikubwa hasa katika sekta
ya michezo.
Alieleza kuwa vijana wamewezeshwa katika shughuli
za kiuchumi kwa kupatiwa vifaa mbali mbali vya kujiendeleza pamoja na kupatiwa
nafasi za mafunzo kazi ili kuweza kujiajiri wenyewe kwa lengo la kuinua pato lao na la Taifa.
Kwa upande wa utamaduni, Balozi Karume alisema
kuwa Wizara imeendelea kuazimisha matamasha mbali mbali likiwemo tamasha la
utamaduni wa Mzanzibari, kukiendeleza kikundi cha Taifa cha taarab kwa
kukipatia vifaa na ofisi.
Akieleza kuhusu lugha ya Kiswahili alisema kuwa kongamano
la Kimataifa la lugha hiyo limekuwa likifanyika kwa kushirikisha wataalamu na
magwiji wa lugha hiyo kutoka ndani na nje ya nchi na kueleza jinsi Wizara hiyo
inavyokuza michezo ya asili.
Aidha, Wizara hiyo ilimpongeza Rais Dk. Shein kwa
azma yake ya kuanzisha Studio ya Filamu na Muziki iliyopo Rahaleo ambapo wasanii, Taasisi za
Serikali pamoja na watu binafsi wamekuwa wakiitumia kwa shughuli mbali mbali za
Sanaa na kijamii.
Aliongeza kuwa Wizara hiyo imefanikiwa kuzindua program ya
Ajira kwa Vijana kwa awamu ya kwanza ambapo jumla ya vijana 3,300 (Unguja 2,102
na Pemba 1,198) wamenufaika na programu hiyo.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment