Habari za Punde

Innaa Lillaahi Wainnaa ilayhi Raajiuun: Waziri Kiongozi wa Kwanza Ramadhan Haji Faki Afariki Dunia Jana Jijini Dar es Salaam na Kuzikwa Leo Kijiji Kwao Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Waziri Kiongozi wa kwanza Brigedia Jenerali wa JWTZ Mstaafu. Ramadhan Haji Faki afariki dunia jana Jijini Dar es Salaam na Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuzikwa  leo Kijijini kwao Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini Unguja.

Maziko yatafanyika leo na Sala ya kumuombea mwili wa Marehemu itafanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa, Masjid Mushawar Muembeshauri baada ya Sala ya Adhuhuri na kuzikwa kijijini kwao Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Marehemu Brigedia Jenerali Mstaaf na Waziri Kiongozi Ramadhani Haji Faki ni miongozi mwa Watu 14 waliopanga na kufanikisha Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964.

Brigedia Jenerali Ramadhani Haji Faki ni kati ya Wanamapinduzi 14 ambae alibaki hai na pia alikuwa Waziri Kiongozi wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mwenyenziu Mungu amsamehe madhambi yake na kumpa kauli thabiti.

  Innaa Lillaahi Wainnaa ilayhi Raajiuun

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.